Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 18:52

Israel inawapa mafunzo askari wa Saudia

Israel inawapa mafunzo askari wa Saudia
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amefichua kuwa utawala haramu wa Israel unatoa mafunzo ya kijeshi kwa askari wa Saudi Arabia katika mpango wa siri wa uhusiano wa tawala hizo mbili.

Sheikh Naim Qassem amesema maafisa hao Wasaudi wanapata mafunzo kufuatia uhusiano wa siri wa Israel na Saudia ambao sasa umeimarika na kuwa ushirikiano wa kijeshi.

Amebaini kuwa Israel imeamua kuwapa mafunzo askari wa Saudia baada ya utawala wa Saudia kushinikiza Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Barazala la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kuitangaza harakati ya Hizbullah kuwa kundi la kigaidi.

Sheikh Qassem amesema kwa miaka mingi sasa Saudia imejizuia kuwapa mafunzo wanaharakati wa kupigania ukombozi wa Palestina sambamba na kukataa kushirikiana na Iran kwa maslahi ya uthabiti katika eneo.

Siku ya Jumapili, gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post liliripoti kuwa, 'si tu kuwa Israel haijatengwa bali pia sasa imeingizwa katika duara la Saudi Arabia. Sehemu ya mpango huo ni IIsrael kufungua ofisi ya kidiplomasia Abu Dhabi na kuimarisha maingiliano na nchi za Ghuba ya Uajemi."

Gazeti hilo limeongeza kuwa, Saudia na waitifaki wake wanataka msaada wa Israel katika kukabiliana na Iran.

Mwezi Juni mwaka jana kulifichuka ripoti kuhusu mikutano kadhaa ya siri baina ya wawakilishi wa Saudi Arabia na Israel kwa lengo la kujadili njia za kukabiliana na Iran.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg, mikutano hiyo imefanyika mara tano katika kipindi cha miezi 17 katika mwaka 2014-1015 ambapo maafisa hao wa Saudia na utawala haramu wa Israel walikutana nyakati mbali mbali huko India, Italia na Jamhuri ya Czech.

Aidha mapema mwezi Juni mwaka jana maafisa mashuhuri wa zamani wa Saudia na Israel walikutana katika taasisi ya Council on Foreign Relations huko Washington. Kikao hicho kilihudhuriwa na Anwar Majed Eshki, mshauri wa zamani wa serikali ya Saudia, na Dore Gold balozi wa zamani wa Israel aliye karibu na Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …