Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 24 Aprili 2016 19:18

Syria yailaumu Saudia kwa kuvuruga mwafaka wa kusimamisha vita

Syria yailaumu Saudia kwa kuvuruga mwafaka wa kusimamisha vita
Waziri wa Habari wa Syria ameilaumu Saudi Arabia na baadhi ya waitifaki wake kwa kuvuruga makubaliano ya kusimamisha vita nchini Syria.

Mtandao wa habari wa al Nashra wa nchini Lebanon, leo umemnukuu Omran al Zoubi akisema kuwa, Saudia, Uturuki na Qatar zimeyaamrisha makundi ya kigaidi kuirejesha hali ya Syria katika hali iliyokuwa nayo kabla ya makubaliano ya kusimamisha vita.

Amesema, jinai zinazoendelea kufanywa na waasi ndani ya Syria zinaonesha namna waasi hao walivyoshindwa kukabiliana na wanaejshi wa Syria katika medani za mapambano na pia kushindwa waasi hao kufikia malengo yao haramu kupitia mazungumzo.

Mwafaka wa kusimamisha vita baina ya jeshi la Syria na waasi ulianza kutekelezwa tarehe 27 Februari kwa msaada wa Russia na Marekani.

Magenge ya kigaidi ya Daesh (ISIS) na Jabhat al Nusra ambayo kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni magenge ya kigaidi, hayakushirikishwa kwenye mwafaka huo kama ambavyo hayashirikishwi pia katika mazungumzo ya amani ya Syria.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …