Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 22 Aprili 2016 12:07

Kuanza duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Yemen huko Kuwait

Kuanza duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Yemen huko Kuwait
Baada ya wiki kadhaa za mvutano hatimaye, mazungumzo ya kusaka amani kwa ajili ya kumaliza mashambulio ya miezi 13 ya kundi linalojiita Muungano wa Kiarabu linaloongozwa na Saudia Arabia yalianza jana usiku hukoo Kuwait.

Mazungumzo hayo yalikuwa yaanze tarehe 18 mwezi huu wa Aprili hukohuko Kuwait lakini yalisimama kufuatia malalamiko ya harakati ya wananchi ya Ansarullah kuhusiana na ukiukaji wa Saudi Arabia wa mapatano ya usitishaji vita. Usitishaji vita huo ambao unasimamiwa moja kwa moja na Umoja wa Matifa tokea Aprili 10, hukiukwa mara kwa mara na muungano uliotajwa unaoongozwa na Saudi Arabia, kama ambavyo saa chache kabla ya kuanza mazungumzo ya hivi sasa huko Kuwait pia ripoti za kuaminika zilithibitisha kuwa ndege za kijeshi za Saudia zilishambulia maeneo kadhaa kaskazini mwa Yemen, kinyume na mapatano ya usitishaji vita. Hii ni katika hali ambayo duru iliyopita ya mazungumzo ya amani ya Yemen huko Uswisi ilivunjika kufuatia ukiukaji kama huo wa Saudia.

Pamoja na hali hiyo, Ismail Walad as-Sheikh Ahmad, mwakilishiwa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea masikitiko yake mwanzoni mwa duru hii ya mazungumzo huko Kuwait, ambayo yanawashirikisha wawakilishi wa Ansarullah na wa Chama cha Congress cha serikali iliyostaafu ya Yemen, kuhusiana na matokeo ya mashambulio ya umwagaji damu dhidi ya Yemen, na kuzitaka pande zinazopigana zishirikiane ili kufikia mapatano ya kudumu ya kumaliza vita nchini humo. Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba umoja huo unasisitiza juu ya kufanyika mazungumzo hayo ukiwa na matumaini ya kumalizwa vita na kufikiwa amani ya kudumu kati ya makundi yote ya Yemen. Huku ikisisitiza juhudi kubwa inazofanya kwa ajili ya kupatikana amani ya kudumu nchini Yemen licha ya uchochezi na ukiukaji usitishaji vita unaofanywa na Saudia nchini humo, harakati ya Ansarullah imesema kuwa lengo lake kuu katika mazungumzo ya Kuwait ni kusimamisha kabisa mabshambulio dhidi ya Yemen na kisha kufanya mazungumzo ya kisiasa na makundi yote ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti, tokea kuanza kwa mashambulio ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen hapo tarehe 26 mwezi Mchi 2015, kwa lengo la kumrejesha kwa nguvu madarakani rais aliyestaafu na mtoro wa nchi hiyo, hadi sasa Wayemen wapatao elfu kumi, wengi wao wakiwa ni raia wakawaida na hasa wanawake na watoto wodogo wameuawa katika hujumu hiyo ya kichokozi. Kwa mujibu wa ripoti hiyohiyo, zaidi ya asilimia 80 ya miundombinu muhimu ya nchi hiyo zikiwemo hospitali, shule, barabara na vituo vya umeme na maji ya kunywa imeharibiwa katika hujumahiyo. Mazungumzo ya Kuwait yanafanyika katika hali ambayo harakati ya wananchi ya Ansarullah na jeshi la Yemen bado wanadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Yemen ukiwemo mji mkuu, San'aa na hivyo kuvunja harakati zote za kisiasa na kijeshi za Saudia na washirika wake za kutaka kuirejesha madarakani serikali iliyojiuzulu.

Kwa kuzingatia natija ndogo ya mazungumzo yaliyopita kati ya wawakilishi wa Ansarullah, Chama cha Congress na serikali iliyojiuzulu ya Yemen, inatazamiwa kuwa mara hii pande zinazozozana zitajitahidi kulegeza misimamo yao ili kuandaa mazingira ya kufikiwa mapatano ya kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Licha ya kuwepo matumaini hayo lakini bado kuna uwezekano wa kutokea chochote katika mazungumzo hayo ya Kuwait.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …