Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 21 Aprili 2016 09:53

Rouhani na al Abadi wajadili mapambano dhidi ya ugaidi

Rouhani na al Abadi wajadili mapambano dhidi ya ugaidi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri Mkuu wa Iraq wamefanya mazungumzo ya simu wakijadili hali ya sasa ya Mashariki ya Kati husuan mipango ya serikali ya Iraq ya kurejesha amani nchini humo na kupambana na ugaidi.

Rais Hassan Rouhani amesema katika mazungumzo hayo kwamba, kupambana na makundi ya kigaidi hususan lile la Daesh ni wadhifa wa nchi zote zinazowajibika diniani na kuongeza kuwa, Iran itaendelea kuwa bega kwa bega na serikali na wananchi wa Iraq katika kupambana na makundi hayo.

Rais Rouhani amempongeza Waziri Mkuu wa Iraq kutokana na ushindi wa hivi karibuni wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi na kusema: Jamhuri ya Kiislamu inatambua amani na usalama wa Iraq kuwa ni amani na usalama wake na itafanya jitihada zote kuimarisha usalama nchini Iraq.

Rais Hassan Rouhani pia amezitaka nchi mbalimbali kuacha nara tupu na kuingia katika awamu ya vitendo katika suala la kupambana na ugaidi na kusema: Inasikitisha kwamba baadhi ya nchi zinazodai kupambana na ugaidi zingalia zinatoa misaada ya silaha na kununua mafuta kutoka kwa kundi la kigaidi la Daesh.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh ni tishio kwa eneo la Mashariki ya Kati na maeneo mengine ya dunia na kusema, taifa na serikali ya Iraq inapongeza msimamo imara wa Iran katika kupambana na Daesh. Vilevile amesisitiza udharura wa kuimarishwa zaidi ushirikiano wa pande hizo mbili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …