Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 20 Aprili 2016 18:58

Umoja wa Mataifa yazitaka pande zote nchini Syria kufungamana na mazungumzo ya amani

Umoja wa Mataifa yazitaka pande zote nchini Syria kufungamana na mazungumzo ya amani
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zote hasimu nchini Syria kufungamana na mazungumzo ya amani ya Syria ya Geneva Uswisi.

Stephane Dujarric amezungumzia matukio ya Syria na ukosiaji wa wapinzani wa Syria kwa utendaji wa Umoja wa Mataifa nchini humo na kusema kwamba, mazungumzo ya Geneva ni mazungumzo nyeti kabisa yanayofanyika kwa kuhudhuriwa na Umoja wa Mataifa na kwamba, umoja huo unazitaka pande zote hasimu kufungamana na mazungumzo hayo.

Stéphane Dujarric ameongeza kuwa, pande zote nchini Syria zinapaswa kuheshimu suala la kuweka kando uhasama na uadui ili Umoja wa Mataifa uweze kuisaidia zaidi nchi hiyo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesifu utendaji wa mwakilishi maalum wa UN katika masuala ya Syria na kueleza kuwa, utendaji wake umekuwa mzuri.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika majuma ya hivi karibuni jeshi la Syria limepata mafanikio makubwea katika operesheni yake ya kuikomboa miji na maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya waasi.

Ripoti zinaeleza kuwa, hali ya amani na utulivu inaonekana ikianza kurejea taratibu katika baadhi ya miji.

Imeelezwa kuwa, wakimbizi wa Syria zaidi ya milioni moja wamerejea majumbani mwao baada ya amani na utulivu kurejea katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa serikali ya Syria ameeleza kuwa, raia karibu milioni moja na laki saba wa nchi hiyo wamerejea katika makazi yao baada ya hali ya utulivu kurejea katika miji kadhaa ya nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …