Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 20 Aprili 2016 18:33

Daesh watumia silaha za kemikali dhidi ya raia kaskazini mwa Iraq

Daesh watumia silaha za kemikali dhidi ya raia kaskazini mwa Iraq
Wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, wametumia silaha za kemikali katika maeneo ya raia kaskazini wa Iraq.

Shambulizi hilo limefanywa katika eneo la Abu Shit wanapoishi idadi kubwa ya Wakurdi katika viunga vya mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq ambapo magaidi hao wametumia maguruneti yenye silaha hizo zilizopigwa marufuku. Kwa mara kadhaa sasa wanachama wa kundi hilo la kitakfiri wamekuwa wakitumia silaha zenye gesi ya sumu katika maeneo ya raia wa kawaida na kuua idadi kubwa ya watu. Katika hatua nyingine, Abdul-Muhsin al-Abbasi, mmoja wa makamanda wa jeshi la Iraq ametangaza kuwa, askari wa nchi hiyo kwa kushirikiana na wapiganaji wa kujitolea, wamefanikiwa kukomboa vijiji kadhaa vya mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa nchi. Katika operesheni hizo, jeshi la Iraq limemuua kiongozi wa ngazi za juu kabisa wa kundi la Daesh aliyekuwa akiitwa Yassin al-Khalifawi, maarufu kwa jina la Da'fasah, akiwa pamoja na viongozi wengine wa genge hilo la kigaidi. Aidha askari wa Iraq pia wamedhibiti silaha na zana kadhaa za kijeshi zilizokuwa zikitumiwa na matakfiri hao maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu. Hayo yanajiri katika hali ambayo, ndege za kijeshi za Uturuki kwa mara nyingine tena zimefanya mashambulizi kadhaa ndani ya ardhi ya Iraq katika maeneo ya wapiganaji wa Kundi la PKK ambao wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa Daesh nchini humo. Hii si mara ya kwanza kwa ndege za Uturuki kuvuka mipaka yake na kutekeleza hujuma zake nje ya nchi hiyo, suala ambalo limekuwa likilaaniwa na serikali kuu ya Baghdad.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …