Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 20 Aprili 2016 12:31

Iran, Kazakhstan zatoa wito wa kupambana na ugaidi

Iran, Kazakhstan zatoa wito wa kupambana na ugaidi
Maspika wa Mabunge ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kazakhstan wametoa wito wa kuwepo juhudi za pamoja na za dhati za kukabiliana na makundi ya kigaidi na haswa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika eneo hili la Mashariki ya Kati.

Ali Larijani, Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran na mwenzake wa Kazakhstan Kabilullah Dzhakupov waliyasema hayo jana katika mji mkuu wa Russia, Moscow, pambizoni mwa mkutano wa maspika wa mabunge ya Eurasia. Wamesema harakati za makundi ya kigaidi haziwezi kutokomezwa bila ushirikiano na irada ya kisiasa.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Iran amesema mabunge ya nchi mbili hizo yana nafasi nzuri katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyuga tofauti.

Dzhakupov kwa upande wake amesema anaamini kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina umuhimu sio tu katika masuala ya eneo bali kote duniani.

Kadhalika amemualika Ali Larijani, Spika wa Bunge la Iran kushiriki kongamano lenye kaulimbiu "Dini dhidi ya Ugaidi" litakalofanyika katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana, mnamo Mei 31.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …