Chapisha ukurasa huu
Jumatano, 20 Aprili 2016 12:18

Merkel aikosoa Israel kwa ujenzi wa vitongoji Palestina

Merkel aikosoa Israel kwa ujenzi wa vitongoji Palestina

Chansela wa Ujerumani amekosoa hatua ya utawala haramu wa Israel ya kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu na kusema kuwa ujenzi huo unazuia mchakato wa amani.

Chansela Angela Merkel, wa Ujerumani aliyasema hayo jana Jumanne katika mazungumzo na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani wa Palestina mjini Berlin na kuongeza kuwa, sera hiyo ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni haitakua na tija nyingine ghairi ya kukwamisha kile kinachotajwa kuwa 'suluhu ya kubuniwa mataifa mawili.' Kwa upande wake Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema ujenzi wa viongoji vya walowezi wa Kizayuni sambamba na kubomoa nyumba za Wapalestina, ni katika changamoto kuu zinazokwamisha uhuru wa taifa la Palestina.

Kauli ya Merkel inajiri katika hali ambayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amekosoa vikali hatua ya Israel kuendeleza ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Akizungumza mbele ya Baraza la Usalama hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alibainisha wasiwasi wake kuhusu Israel kuendelea kubomoa nyumba za Wapalestina na kusema mazingira yanayotawala sasa yametatiza juhudi za kupatikana amani.

Alisema kubomolewa nyumba za Wapalestina na kujengwa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni mambo yanayoibua maswali kuhusu iwapo lengo la Israel ni kuwatimua Wapalestina kutoka maeneo kadhaa ya Ukingo wa Magharibi na hatimaye kuzuia kuundwa taifa huru la Palestina.

 

 

Maandiko yanayofanana

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)