Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

 

Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wako mjini Bujumbura, Burundi 

wakikutana kwa mazungumzo na pande tafauti zinazo husika na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo. 

Hata hivyo Waziri wa Tanzania anaye husika na Jumuiya ya Afrika Masariki Harrison Mwakyembe amesema kuwa, mawaziri hao hawana madaraka ya kuingilia maamuzi ya kisheria ya nchi nyingine. 

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa zaidi……….bonyeza hapa..

 

 

Nchini Kenya huenda wenye kutekeleza nauaji dhidi ya watu wanaotuhumiwa kwa uchawi wakajikuta pabaya, iwapo mswada unaonuia kuifanyia marekebisho sheria ya uchawi  utapasishwa na kuwa sheria rasmi. Hii ni baada ya kukithiri kwa visa vya kuuawa kwa kuteketezwa moto kwa washukiwa wa uchawi katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo, zikiwemo kaunti za Kilifi, Kwale, Machakos, Makueni, Kisii na Siaya.

Mwandishi wetu wa Nairobi Hussein Hassan amezungumza na Mbunge aliyeuandaa mswada huo na kutuandalia taarifa ifuatayo…….bonyeza hapa/

Mufti Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Issa Bin Shaaban Simba,  amefariki dunia jana alfajiri katika hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam nchini humo alipokwenda kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya moyo. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara  ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Waislamu wote nchini humo kufuatia kifo hicho.

Mwandishi wetu Grayson Gideon na taarifa zaidi bonyeza hapa kwa taarifa zaidi…../

 

Familia za watu waliotiwa mbaroni katika vurugu za mwanzoni mwa mwaka huu, huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia hatua ya serikali kutaka kuifanyia marekebisho katika ili kutoa mwanya kwa Rais Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani, wameitaka serikali kufukua kaburi la umati la eneo la Maluku, kando na mji mkuu Kinshasa, ili kubaini kupitia vipimo vya unasaba DNA kama waliozikwa humo ni ndugu zao au laa! Hayo yamekuja kufuatia familia hizo kutiwa wasi wasi mkubwa baada ya kupita muda mwingi bila ndugu zao waliotiwa mbaroni na polisi katika vurugu hizo, kutojulikana walipo kwa muda mrefu sasa.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi kwa kubonyeza hapa chini

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameidhinishwa rasmi na chama chake kugombea urais visiwani Zanzibar. 

Tangazo la kuidhinishwa Maalim Seif kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho lilitangazwa jana Jumamosi na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika viwanja vya demokrasia vya Kibanda Maiti mjini Unguja.

Mwandishi wa Radio Tehran amehudhuriwa mkutano huo na kutuandalia ripoti hii hapa chini:

Siku moja baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutangaza kuwa serikali yake itazindua mikakati mipya ya kukabiliana na ugaidi na wimbi la vijana kushawishiwa kujiunga na makundi yenye misimamo mikali, wakuu wa usalama wamefanya mkutano wa dharura kujadili kadhia hiyo. Aidha mkutano huo umegusia uwezekano wa taifa hilo la Afrika Mashariki kuangalia upya suala la iwapo liondoe jeshi lake la KDF kutoka nchini Somalia au la.

Bonyeza hapa kumsikiliza mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan kwa maelezo zaidi………./

Kongamano la 11 la Kimataifa la Itikadi ya Imam Mahdi AS limemalizika Jumatatu hapa mjini Tehran na kushirikisha pamoja shakhsia mbalimbali wa ndani na nje ya Iran
Shakhsia mbalimbali wameshiriki kwenye kongamano hilo la siku mbili ambalo lilimalizika kwa kutoa wito wa kuwepo ushirikiano na umoja wa Waislamu duniani. Kulikuwa na washiriki wa ngazi mbalimbali wa Iran pamoja na wanafikra kutoka nchi zaidi ya 52 duniani wakiwemo wanazuoni kutoka bara Afrika. Kati ya washiriki hao alikuwa Sheikh Hassan Salim ambaye amezungumza na Mubarak Henia na kwanza kabisa anafafanua kuhusu kikao hicho. Kusikiliza bonyeza HAPA.../

Eneo la maegesho ya feri kusini mwa mkoa wa pwani nchini Kenya, lametajwa kama eneo baya zaidi kwa ukandamizaji wa haki za wanawake. Hayo yamejiri baada ya kubainika kuwa, wanawake wamekuwa wakifanyiwa vitendo vichafu ikiwemo kutomaswa miili yao na wanaume ajenabi wakati wanawake hao wawapo katika foleni ya kusubiria pantoni. Licha ya sheria kali za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kuwepo, lakini wanawake wengi ambao hukumbwa na vitendo hivyo wamekuwa wakiogopa hata kuripoti kwenye vyombo husika kutokana na vitisho wanavyovipata kutoka kwa wahusika wa dhulma hizo. 

Bonyeza hapo chini kujiunga na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa taarifa zaidi………../

Serikali ya Rwanda imetangaza kuifunga jumla idhaa ya Kinyarwanda ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC. Uamuzi huu umefuatia kusimamishwa kwa muda matangazo ya shirika hilo kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu baada ya shirika hilo kukejeli mauaji ya umati ya mwaka 1994 nchini Rwanda. Sakata hili ilianza tangu tarehe Mosi mwezi wa kumi mwaka jana wakati televisheni ya BBC iliporusha makala maalum kuhusu mauaji ya Rwanda.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi…../

 

Inaelezwa kuwa, wanafunzi wengi wa kike mjini Mombasa nchini Kenya wamekuwa wakiogopa kupata mimba wakiwa masomoni zaidi ya khofu yao kwa ugonjwa hatari wa ukimwi. Ripoti kutoka mjini Mombasa, zinasema kuwa, wazazi nao wamekuwa wakichangia kwa asilimia katika suala hilo, ambapo huwa wanawasaidia mabinti zao kutumia king aya kuzuia mimba, ili wasipate aibu ya kushindwa kuendelea na masomo. Wanasema ni bora ukimwi kuliko mimba, kwa kuwa mimba huwa haifichiki kwa watu.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa Seifullah Murtadha kwa taarifa zaidi………………../