Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Jumanne ya wiki hii taifa la Burundi lilifanya uchaguzi ambao mbali na kususiwa na viongozi wa upinzani, ulisusiwa pia na jamii ya kimataifa, baada ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, kugoma kuwatuma waangalizi wao kwenda nchini humo kufuatilia zoezi hilo. Hata hivyo hatua hiyo haikuwaeza kudhoofisha azma ya serikali ya chama tawala madarakani CNDD-FDD, kuweza kuahirisha uchaguzi huo kama ilivyoamriwa na jamii ya kimataifa. Tayari tume ya uchaguzi nchini Burundi, imetangaza matokeo ya uchaguzi huo kuwa Rais Pierre Nkurunziza, ameongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya mahasimu wake, huku tume hiyo ikiahidi kutangaza rasmi matokeo hayo jioni ya Ijumaa hii. Ili kujadili kwa upana kuhusiana na uchaguzi huo mkuu nchini Burundi, mwenzetu Sudi Jafar amefanya mahojiano na Minani Rajabu Ali, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa jijini Bujumbura ambaye ameanza kuzungumzia hali halisi ya kadhia hiyo……./

Safari ya Rais Barack Obama wa Marekani inayotarajiwa kuanza Ijumaa wiki hii inaendelea kuibua hisia tofauti. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema, Nairobi imeandaa mazingira ya kutosha kuhusu kumpokea raia huyo wa Marekani. Hiyo itakuwa ni ziara yake ya kwanza nchini Kenya tangu awe rais wa Marekani.

Ikumbukwe kuwa baba wa Barack Obama ni Mkenya na rais huyo wa Marekani mara ya mwisho kuitembelea Kenya ilikuwa ni mwaka 2006 wakati alipokuwa Seneta wa jimbo la Illinois.

Mwandishi wa Radio Tehran jijini Nairobi ametuandalia ripoti ifuatayo:

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamefanya maandamano kupinga muswada uliowasilishwa na Rais Catherine Samba-Panza wa nchi hiyo, unaowazuia raia wa taifa hilo walioko nje kutoshiriki kujiandikisha wala kupiga kura katika uchaguzi ujao. Kwa mujibu wa waandamanaji, muswada huo, unalengo la kuwazuia Waislamu ambao ndio wengi walioko nje, kutoshiriki katika zoezi hilo ambalo ni haki yao ya msingi.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati, Mosi Mwasi kwa taarifa zaidi…bonyeza hapa chini…………/

Chama tawala nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao.  Dkt Magufuli, alijipatia kura 2104 ikiwa ni sawa na asilimia 87 % ya kura za wajumbe kwenye mkutano mkuu wa chama hicho mjini Dodoma.  Bi Amina Salum Ali alimaliza katika nafasi ya pili akiwa na kura 253 ambayo ni sawa na asilimia 10.5 % ya kura zote  huku Dkt. Asha-Rose Migiro akikunja jamvi la tatu bora kwa kujizolea asimilia tatu ya kura ya wajumbe ama kura 59. Kufuatia ushindi huo Daktari Magufuli ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Magufuli amemteua Samia Suluhu Hassan kutoka Visiwani Zanzibar kuwa mgombea mwenza.

Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Grayson Gideon.

Serikali ya Burundi imemkataa mwanadiplomasia wa pili wa Umoja wa Mataifa aliyechaguliwa hivi karibuni kusaidia juhudi za kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo ikisema kuwa, mwanadiplomasia huyo hajaonyesha ushirikiano wowote na serikali ya Bujumbura. Aidha serikali imemkosoa mpatanishi huyo kwamba, tangu alipowasili nchini humo hajaweza kujitambulisha kwa serikali kama vile ambavyo ameshindwa pia kukutana na Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamida Issa kwa taarifa zaidi…bonyeza kwa chini kupata sauti……../

Wimbi la bidhaa feki za chakula na dawa limezidi kuipa changamoto serikali ya Tanzania baada ya mamlaka kukiri kukithiri kwa uingizwaji wa bidhaa bandia nchini humo licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya nchi hiyo. Wakati mamlaka ya chakula na dawa nchini humo TFDA ikisema inafanya juhudia kupambana na uuzwaji wa bidhaa bandia za vyakula na dawa , Redio Tehran imeshuhudia bidhaa hizo zikiendelea kuuzwa katika soko kuu la biashara Kariakoo jijini Dar es salaam.

Mwandishi wetu Grayson Gideon ana taarifa zaidi…hapa chini………../

Wakristo nchini Kenya, wameitaka serikali kukabiliana na wahubiri wa urongo wanaojiita kwa majina ya Manabii huku wakitumia nguvu za giza kutapeli umma. Hayo yamejiri kufuatia kuongezeka vitendo vya utapeli vinavyofanywa na watu hao kwa madai ya kuwaongezea kipato waumini hao na kisha kuwaibia kabisa pesa walizokuwa nazo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa taarifa zaidi… bonyeza hapa chini………/

Jumatano, 01 Julai 2015 17:08

Mashindano ya Qur'ani Tukufu nchini Uganda

Mashindano ya Qur'ani Tukufu yamefanyika tena nchini Uganda katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kama ilivyokuwa mwaka jana. Mashindano hayo yanadhaminiwa na kusimamiwa na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Kampala.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano ya Qur'ani Tukufu, mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail ametutayarishia ripoti ifuatayo.

 

Huenda ndoto ya muda mrefu ya walimu wa Kenya kutaka nyongeza ya mshahara ikatimia, baada ya mahakama moja nchini humo kuagiza wapewe nyongeza ya kati ya 50% na 60%.

Walimu hao wamekuwa wakishiriki migomo na maandamano ya mara kwa mara bila mafanikio.

Mwandishi wetu wa Nairobi Hussein Hassan ametutumia taarifa ifuatayo...

Licha ya kususia uchaguzi wa serikali za mitaa na bunge ulaofanyika Jumatatu Juni 29, 2015 nchini Burundi, Muungano wa "Amizero ya Abarundi" unaoundwa na FNL ya Agathon Rwasa na Uprona ya Charles Nditije waonekana kuchukuwa nafasi ya pili katika matokeo ya awali yanaoendelea kutolewa na tume za mikoa na tarafa. Mwandishi wa Radio Tehran Amida ISSA amemuhoja kiongozi wa chama cha FNL, Agathon Rwasa, kutaka kujuwa endapo ataridhia matokeo ya mwisho au la?

Ingia hapa chini kusikiliza mahojiano hayo.