Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanapitia wakati mgumu, baada ya magaidi wa Kikristo wa Anti-Balaka kuanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya jamii ya Waislamu katikati mwa nchi hiyo. Aidha mashambulizi ya magaidi hao yanatajwa kukwambisha uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi wa Oktoba mwaka huu.  Mbali na hujuma za wanachama wa kundi hilo, Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini humo, imetangaza kukosekana maandalizi muhimu kwa ajili ya zoezi hilo muhimu, suala ambalo limewafanya wananchi kuamini udhaifu huo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya kati Mosi Mwasi kwa habari kamili…Bonyeza kwa chini ili kupata sauti……./

Serikali ya Kenya imepata pigo baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kuitaka iwape walimu nyongeza ya mshahara ya hadi asilimia 60 kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti. Awali, Tume ya Kuajiri Walimu TSC ilikuwa imeenda mahakamani kupinga agizo hilo, ikisisitiza kuwa serikali haina pesa za kuwapa walimu nyongeza hiyo. Kwa upande wao walimu wamepokea kwa mikono miwili hukumu ya mahakama hiyo wakisisitiza kuwa, imekuja wakati mwafaka na hivyo haitakiwi kukatiwa tena rufaa na serikali ili kubatilishwa.

Mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan ana maelezo zaidi…Bonyeza chini kupata sauti……/

Uchaguzi wa viongozi wa mitaa nchini Burundi umefanyika Jumatatu hii, huku ukishuhudia ushiriki duni. Viongozi serikalini wameutaja uchaguzi huo kuwa muhimu kwa nchi hiyo huku wakiwataka wananchi kuwapigia kura viongozi wanaowaona kuwa wanaoweza kutatua matatizo yao. Hayo yanajiri katika hali ambayo zaidi ya vijana 200 wametiwa mbaroni leo hii, kwa tuhuma kwamba walikuwa wakipanga kujiunga na makundi ya uasi dhidi ya serikali ya Bujumbura.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa zaidi……bonyeza chini kupata sauti…./

Wataalamu wa masuala ya kisiasa na wananchi huko nchini Tanzania wamekosoa kauli ya rais mstaafu wa awamu ya tatu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi pale alipowatusi viongozi wa upinzani kwamba, ni wapumbavu na malofa. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, kauli hiyo haikutarajiwa kutolewa na shakhia kama huyo na hasa kwa kuzingatia kuwa tayari Tume ya Uchaguzi nchini humo, imekwishapiga marufuku kwa wagombea kutoa kauli chafu katika kipindi chote cha kampeni za urais ujao.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar-es-Salaam, Tanzania Omar Manji kwa taarifa kamili…bonyeza chini kupata sauti………/

Nchini Kenya malumbano miongoni mwa wanasiasa kuhusu makubaliano ya biashara ya sukari kati ya nchi hiyo na Uganda yameendelea kushuhudiwa, huku upinzani ukitazamiwa kuanza mikutano ya hadhara Jumatano hii katika maeneo ya Magharibi na Nyanza kuhusu suala hilo. Baadhi ya wanasiasa wamemkosoa kinara wa upinzani, Raila Odinga kwa kuendesha kampeni ya kuipinga serikali, huku wengine wakitangaza uugaji wao mkono kwa serikali hiyo ya Nairobi

Kwa maelezo zaidi tumtegee sikio mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan……Bonyeza chini upate sauti……/

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé amerejea nchini humo kwa siri, ili kuweza kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea urais. Bozizé amerejea nchini humo, licha ya kuwepo indhari ya serikali ya kumtia mbaroni kutokana na kutenda jinai dhidi ya binaadamu. Hata hivyo mwanasiasa huyo, amepuuza indhari hizo na ameahidi kushiriki katika uchaguzi huo bila ya wasi wasi wowote.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati, Mosi Mwasi kwa taarifa kamili…Bonyeza chini upate sauti…../

Watanzania wametakiwa kuwa watulivu na makini zaidi wakati Wizara ya Afya ya nchi hiyo ikiendelea kufanya uchunguzi wa vipimo vya mtu anayesadikiwa kufariki dunia kwa ugonjwa hatari wa Ebola, mkoani Kigoma. Kufuatia taarifa hiyo, Watanzania wamepatwa na hali ya taharuki juu ya ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa umepelekea maelfu ya watu kupoteza maisha katika nchi za magharibi mwa Afrika. Wizara ya Afya nchini Tanzania, imewataka watanzania kutoa taarifa mapema katika vituo vya afya pindi watakapogundua mtu mwenye dalili za ugonjwa huo hatari.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salam, Omar Manji kwa taarifa kamili……bonyeza hapa chini kupata sauti…./

Huenda viongozi kadhaa wa kisiasa wa kaunti ya mombasa nchini Kenya wakatiwa mbaroni ili kuhojiwa kufuatia kile kinachodaiwa na idara ya usalama ya nchi hiyo kuwa ni Uchochezi wa jamii. Sakata hilo limekuja baada ya kufichuliwa kuwepo kampeni za kuwataka wananchi kutojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa Seifullah Murtadha kwa taarifa zaidi…bonyeza hapa chini upate sauti…../

Vijana wa Kiislamu nchini Kenya wameendelea kushuhudia kero itokanayo na kuhangaishwa hasa pale wanaposaka vitambulisho vya kitaifa kwa ajili ya shughuli nyingine muhimu. Hayo ni baada ya serikali kuahidi kulitatua tatizo hilo muda mrefu uliopita. Kufuatia hali hiyo, jamii ya Wanubi imetishia kuishtaki serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo kutokana na kero hizo, zilizowafanya vijana wengi kukosa nafasi za ajira na kujiendeleza kimasomo nje ya taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan ana maelezo zaidi…bonyeza hapa chini upate sauti……/

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amewataka raia wa nchi hiyo kuwa na subira kwa kutolipiza kisasi cha kuuawa Jenerali Adolphe Nshimirimana katika shambulio la Roketi asubuhi ya Jumapili hii eneo la Kamenge, jijini Bujumbura. Rais Nkurunziza, amesema kuwa wananchi wanatakuwa kuwa makini ili wasiingie katika mtego ambao unaweza ukawa umeandaliwa kwa lengo la kuwachochea Warundi kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamida Issa kwa taarifa zaidi…bonyeza hapa chini upate sauti……../