Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Mapigano baina ya wanachama wa kundi la kigaidi la Anti-Balaka huko mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati yameendelea kushuhudiwa kwa siku kadhaa sasa na kusababisha vifo na majeruhi. Kwa mujibu wa mashuhuda, mapigano hayo yaliibuka baada ya wanachama wa Anti-Balaka walioshiriki mazungungumzo ya amani mjini Nairobi, Kenya kujiunga na wa upande wa pili wa Seleka, huku wakiwataka wenzao kujiunga katika mkondo wa amani, suala ambalo linatajwa kuwa chanzo cha mapigano hayo. Tumezungumza na Mosi Mwasi, ripota wa Redio Tehran katika eneo la Afrika ya Kati na tumeanza kwa kumuuliza……Bonyeza hapa chini kupata Sauti......…../

 

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania zimeendelea kupamba moto ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo hapo tarehe 25 mwezi huu. Katika kampeni hizo wagombea urais wa pande zote wameendelea kutoa ahadi mbalimbali kwa wananchi sambamba na kunadi vipaumbele vyao ikiwa watachaguliwa. Huko Zanzibar Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, hakuwa mbali na ahadi hizo ambapo ameelezea maisha bora kwa wakazi wa visiwa hivyo.

Mwandishi wetu wa Zanzibar, Hassan Issa Ali amefuatilia kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CUF na kutuandalia ripoti ifuatayo……bonyeza chini upate sauti…/

Tukio chungu la maafa ya maelfu ya mahujaji huko mjini Mina, Saudi Arabia hapo tarehe 24 mwezi uliopita wa Septemba, limeendea kuakisiwa zaidi duniani, ambapo shakhsia mbalimbali wameutaja moja kwa moja utawala wa Aal-Saudi kuwa muhusika wa maafa hayo. Kwa mujibu wa weledi wa mambo na shakhsia tofauti waliotoa maoni yao, Saudia imehusika katika maafa hayo kutokana na nchi hiyo kushindwa kuchukua hatua za maana katika kuzuia majanga hayo ambayo yamekuwa yakijikariri karibu kila msimu wa Hija nchini humo. Baadhi ya weledi wa mambo wameikosoa pia nchi hiyo kwa kukataa kusaidiwa kuboresa miundombinu ya ibada hiyo muhimu ya dini ya Kiislamu kwa kile kinachotajwa kuwa ni Aal-Saudi kukhofia kuondolewa madarakani na nguvu ya Waislamu. Tumezungumza na Sheikh Khalifa Khamis, mkuu wa taasisi ya Imam Bukhari ya nchini Tanzania na tulimuhoji…. ..

 

Nchini Tanzania chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, kimepinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete wa nchi hiyo ya kuwataka Watanzania kuondoka majumbani kwao baada ya kupiga kura hapo tarehe 25 ya mwezi huu, na kuitaja kauli hiyo kuwa iliyo kinyume na sheria. Aidha chama hicho kimewataka wafuasi wake  kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura ili kulinda kura zao siku ya uchaguzi huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania. Kufuatia hali hiyo, uongozi wa CHADEMA umekusudia kutuma barua ya mashtaka kwenda taasisi za juu za kimataifa kulalamikia matamshi ya Rais Kikwete.

Kwa taarifa kamili tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Omar Manji…Pata sauti kwa kubonyeza chini……/

Viongozi wa serikali nchini Burundi wametangaza habari ya kutimuliwa mwanadiplomasia wa Rwanda kwa kile walichokisema kuwa ni mienendo hasi ya mwanadiplomasia huyo katika kuchochea machafuko nchini humo. Désire Nyaruhirira, ambaye kwa kipindi cha miaka 10 alikuwa mshauri wa kwanza wa ubalozi wa Rwanda jijini Bujumbura, alitimuliwa hapo jana na viongozi wa serikali ya Burundi. Na taarifa za hivi karibuni zinaarifu kuwa serikali ya Kigali nayo imemtimua balozi wa Burundi nchini Rwanda.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa kamili…….Sauti….

Tatizo la umalaya limekuwa janga kubwa katika nchi nyingi duniani. Huko barani Afrika, tatizo hilo limekuwa linachangia mno kuenea maradhi mbalimbali hasa ugonjwa hatari wa Ukimwi. Kwa nchini Tanzania, viongozi wa kada mbalimbali wanalalamikia suala hilo wakisema linakwamisha juhudi za kupambana na maradhi ya Ukimwi.

Mwandishi wa Radio Tehran na ripoti zaidi.

Waislamu katika pembe mbalimbali duniani wameendelea kuulaumu utawala wa Saudi Arabia kutokana na maafa ya Mina yaliyopelekea Mahujaji zaidi ya 4,000 kupoteza maisha. Wachambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu wanasema kuna haja ya suala la usimamizi wa ibada ya Hija kuwa mikononi mwa jopo la nchi za Kiislamu badala ya Saudia peke yake kama ilivyo hivi sasa. Sheikh Ali Ammar Mwazoa wa Tanga Tanzania ni mwanaharakati wa Kiislamu na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu ambaye alikuwa miongoni mwa Watanzania waliopata tawfiki ya kutekeleza Ibada ya Hija mwaka huu. Salum Bendera amezungumza na Sheikh Ali Ammar ambaye anaanza kuelezea mtazamo wake kuhusiana na maafa ya Mina...

Matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya uchunguzi wa maoni ‘Twaweza’ kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini Tanzania, yameendelea kuwashtua wengi baada ya matokeo hayo kwenda kinyume na vuguvugu la kisiasa. Ripoti ya utafiti huo inayosema kuwa, endapo uchaguzi nchini Tanzania ungefanyika kati ya mwezi Agosti na Septemba, basi mgombea wa CCM, Dk John Pombe Magufuli wa CCM angepata ushindi wa asilimia 65, huku mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Ngoyai Lowassa akipata asilimia 25, mbali na kukosolewa na weledi wengi wa mambo nchini humo, imetajwa kuwa ambayo haikuzingatia pia mlingano na uwiano wa kisiasa. Tumezungumza na Khamis Dambaya, mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania kutoka jijini Dar es Salaam na alikuwa na haya ya kusema…………………Bonyeza chini kupata sauti…/

Hatimaye viongozi wa upinzani nchini Uganda wameamua kumuunga mkono kiongozi mmoja atakayepeperusha bendera yao katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho 2016, ili kukiondoa madarakani chama tawala cha NRM cha nchi hiyo. Hata hivyo weledi wa mambo wametabiri kwamba umoja wa vinara hao wa upinzani, utasambaratika mapema, kwa kile walichosema kuwa ni uroho wa madaraka.

Tujiunge na mwandishi wetu wa nchini Uganda Kigozi Ismail, kwa taarifa kamili…………./

Nchini Kenya kashfa ya kufujwa kwa mamilioni ya pesa katika shirika la huduma kwa vijana NYS imeendelea kuibua hisia mseto ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Ugatuzi na Mipango Ann Waiguru kukiri kuwa shilingi milioni 791 zilipotea katika njia ya kutatanisha. Mbali na hapo Jumatatu hii idadi kubwa ya vijana wanaofanya kazi katika shirika hilo wamemiminika barabarani kulalamikia kile wanadodai kuwa ni kucheleweshwa malipo yao.

Mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan anaripoti zaidi………………/