Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 11 Januari 2012 19:40

Mahojiano na Waziri wa Utamaduni wa Tanzania

Wiki hii Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Emmanuel John Nchimbi ameitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Katika safari yake ya siku tatu hapa mjini Tehran iliyomalizika Jumanne 9 Januari, Iran na Tanzania zilitilaina saini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya utamaduni na sanaa. Waziri Nchimbi ametembelea Iran kwa mwaliko wa Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk. Seyyed Mohammad Husseini.
Akiwa hapa mjini Tehran, Mubarak Henia, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipata fursa ya kuhojiana naye na bofya hapa kupata mahojiano hayo.

 

Huko nchini Kenya, vuguvugu la Mombasa Republican Council MRC linalopigania kujitenga eneo la Mombasa na kuungana na Zanzibar limekanusha kupokea ufadhili wa aina yoyote ile wa kifedha kutoka kwa baadhi wa Wabunge wa Kenya. Tayari serikali ya Kenya imeshalipiga marufukukundi hilo la MRC. Ripoti kamili inapakana kwenye kiungo kifuatacho:

Vuguvugu la kutaka Mombasa kujitenga na Kenya na kujiunga na Zanzibar.

Pia sikiliza:

Jumamosi, 30 Julai 2011 12:37

Sheikh Ahmad Muhdhar Kadhi Mkuu wa Kenya

Mahojiano na Sheikh Ahmad Muhdhar, Kadhi Mkuu wa Kenya, kuhusu mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani 1432 Hijria.

Vile vile sikiliza

Jumanne, 12 Julai 2011 12:47

Ustadh Abdul Wahid Muhammad Yusuf


Mahojiano na Ustadh Abdul Wahid Muhammad Yusuf, hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Malindi, Kenya.

Jumanne, 12 Julai 2011 12:44

Ustadh Ibrahim Ramadhani Shaaban


Mahojiano na Ustadh Ibrahim Ramadhan Shaaban, hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Dar es Salaam Tanzania.

Jumanne, 12 Julai 2011 12:43

Ustadh Saleh Muhammad Ahmad al Ahdal


Mahojiano na Ustadh Saleh Muhammad Ahmad al Ahdal, qari'i na msomaji tajwid kutoka Malindi, Kenya.

Ijumaa, 08 Julai 2011 11:11

Mahojiano na Mh. Najib Balala

Mahojiano na Mheshimiwa Najib Balala, Waziri wa Utalii wa Kenya

Wataalamu mbalimbali wakiwemo wa kidini wamejitokeza visiwani Zanzibar wakiwa tayari kutoa njia mbadala na rahisi zaidi za kuzalisha nishati muhimu ya umeme visiwani Zanzibar. Ifuatayo ni ripoti ya mwandishi wetu wa Zanzibar, Hassan Issa Ali.Unaweza kusikiliza pia kwa kubofya hapa

 

Huko visiwani Zanzibar, kumefanyika semina ya siku tatu ya viongozi wa Serikali ya Zanzibar na watendaji wakuu katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini, nje kidogo ya Unguja Mjini. Rais Ali Mohamed Shein amesema katika ufunguzi wa semina hiyo kuwa viongozi, wanasiasa na watendaji wakuu wa Serikali ya Zanzibar wanatakiwa kuwa na mahusiano na mashirikiano mazuri zaidi ili hatimae kuwe na timu moja yenye ari kubwa ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi. Semina hiyo imefanyika kukiwa na madai kwamba hakuna ushirikiano mzuri kati ya watendaji wa serikali na kuna aina fulani ya kukwamisha mambo na hujuma kutokana na kutofautiana kisiasa watendaji serikalini kama vile Mawaziri na Wakurugenzi wao. Ahmed Rashid amezungumza na Bw. Ismail Jusa Ladhu, Mjumbe katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Bofya hapa kusikiliza sehemu ya pili ya mahojiano hayo.
Sehemu ya kwanza ya mahojiano hayo inapatikana hapa.Page 37 of 37