Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Leo Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amewasilisha bungeni jina la Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano ya nchi hiyo. Uteuzi wa Majaliwa ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi), umewashtua watu wengi hasa kutokana kwamba, tangu awali kulivuma majina ya vigogo wakubwa na maarufu ambao walikuwa wakifikiriwa kuteuliwa katika nafasi hiyo. Baadhi ya watu wameitaja hatua ya Dk Magufuli kwa kumteua Waziri Mkuu huyo kuwa ni hatua moja mbele kuelekea mabadiliko aliyoyaahidi katika kampeni za uchaguzi uliopita hapo tarehe 25 Oktoba. Ili kujadili suala hilo tumezungumza na Khamis Dambaya, mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa jijini Dar es Salaam, ambaye pamoja na kumuelewa vyema Kassim Majaliwa ameanza kwa kutoa tathmini yake juu ya uteuzi huo…………Bonyeza chini kupata sauti./

Zoezi la kuwapokonya silaha kwa nguvu watu  wanaozimiliki kinyume cha sheria linaendelea katika mitaa ambayo imekuwa ikishuhudia usalama mdogo mjini Bujumbura. Kwanye siku ya pili ya operesheni hiyo watu kadhaa wameuwawa katika eneo la Musaga huku hali katika mitaa ya Mutakura na Cibitoke ikiendelea kuwa mbaya kiusalama.
Mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamida Issa na taarifa kamili...

Sherehe za kumuapisha rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli zimefanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa na kimataifa.

Marais kadhaa wa Afrika ambao wamekuwa wakishutumiwa na baadhi ya wapenda demokrasia duniani kwamba hawataki kutoka madarakani wamehudhuria na kushuhudia mchakato wa kidemokrasia wa kuondoka kwa aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na kumkabidhi madaraka rais mpya Dk Magufuli.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jiji Dar es salaam, Omar Manji aliyehudhuria sherehe hizo ……Bonyeza chini kupata Sauti../

 

Kibla ya Kwanza cha Waislamu yaani msikiti mtakatifu wa al Aqsa (Masjidul Aqswa) kiko hatarini hivi sasa kutokana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tumezungumza na Ustadh Ahmad Abdallah Janga wa Tanga, Tanzania ambaye ni mfuatilia na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu na kwa kuanzia anaeleza mtazamo wake kuhusu kushadidi mashambulio ya Wazayuni dhidi ya kibla hicho cha kwanza cha Waislamu katika siku za hivi karibuni.

Ingia hapa chini kupata mahojiano hayo.

Serikali ya Uswidi kupitia ubalozi wake nchini Kenya umetowa kitita cha takriban Shilingi milioni  600  kwa Shirika la Diakonia ili kufadhili mashirika 11 ya kijamii katika kuhamasisha umma kuhusu haki, uongozi bora na uwajibikaji nchini humo. Hii ni katika hali ambayo Kenya imelaumiwa kwa kushindwa kukabiliana na ongezeko la tabaka la baina ya masikini na tajiri nchini humo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Nairobi Suleiman Yeri Ali kwa taarifa kamili………bonyeza kupata sauti…../

Huku wafusi wa chama tawala nchini Tanzania wakiwa katika shamrashamra baada ya Tume ya Uchaguzi nchini humo kumtangaza Muheshimiwa John Pombe Magufuli kama rais wa awamu ya tano ya nchi hiyo, kumekuwa na hali ya wasi wasi wa kutokea ghasia na machafuko kutoka kwa upande wa upinzani. Hii ni kufuatia mgombea wa upinzani Edward Ngoyai Lowassa kukataa matokeo hayo akisema kuwa, yametolewa kwa maslahi ya mgombea wa chama tawala CCM. Hayo yanajiri katika hali ambayo suala la kubatilishwa uchaguzi visiwani Zanzibar, nalo limeendelea kuibua hali ya sintofahamu kwa raia wa Tanzania bara na visiwani. Ili kujadili masuala hayo, tumezungumza na Khamis Dambaya, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya kisiasa nchini humo, na meanza kwa kumuuliza nini tathmin yake kuhusiana na mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia bara na visiwani na alikuwa na haya ya kusema……bonyeza hapa chini kupata sauti…./

Licha ya serikali ya Burundi kutekeleza operesheni za kukusanya silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria, bado suala hilo limeendelea kuwa, changamoto kubwa kwa usalama na amani nchini. Hayo yamejiri kufuatia kuongezeka wimbi la matumizi ya silaha hizo na hivyo kuwafanya wananchi kuzitaja operesheni hizo kuwa zilizofeli.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamida Issa kwa taarifa kamili………bonyeza chini kupata sauti./

Waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi  nchini Tanzania, wametoa tamko lao kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi na zoezi zima la kampeni lilivyokwenda, wakisema kuwa, vyombo vya habari vilitoa upendeleo mkubwa kwa chama tawala CCM. Waangalizi hao wamesema waliangalia vituo vya habari 16 wakati wa kampeni na kubaini kuwa, haki ya upashaji habari katika kampeni zilikuwa zikiminywa na baadhi ya vyombo vya habari kwa maslahi ya CCM ambacho ndio chama tawala Tanzania. Aidha waangalizi hao mbali na kusema kuwa, upigaji kura ulikuwa salama, lakini pia wamekosoa kwa kile walichosema kuwa ni kukosekana haki kidemokrasia kwa pande za upinzani hususan katika kulalamikia matokeo, ikilinganishwa na nchi nyingine za dunia.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Omar Manji kwa taarifa kamili……….bonyeza chini kupata Sauti./

Machafuko yanayoambatana na mauaji yameendelea kushuhudiwa katikati ya mji mkuu Bujumbura, nchini Burundi, huku Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ikikadhibisha kuwepo machafuko hayo na kwamba kile kinachoshuhudiwa ni msako wa jeshi la polisi dhidi ya wahalifu wanaohatarisha usalama jijini hapo.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa ripoti kamili...

Jumatano, 21 Oktoba 2015 14:51

Siku ya Mashujaa nchini Kenya

Sherehe za mashujaa nchini Kenya zimefikia kilele chake leo kwa hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta ambapo kiongozi huyo amewataka wabunge kujiepusha na ubinafsi na badala yake kuwaomba waondoe vipengele tata kwenye mswaada wa Mamlaka ya Bunge wa mwaka 2014.

Mwandishi wa Radio Tehran mjini Nairobi, alihudhuria sherehe hizo na kutuandalia taarifa ifuatayo: