Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 13:34

Rais Uhuru Kenyatta atakiwa kudhibiti matapeli

Rais Uhuru Kenyatta amekokoteza kuwekwa sheria kali kwa viongozi wa kidini wanaoendelea kunyanyasa na kutapeli waumini wao, huku pingamizi kutoka kwa wanasheria na viongozi wa kidini likiendelea kushamiri likiitaka serikali kutumia sheria zilizopo kudhibiti matapeli na viongozi wanaofundisha itikadi kali.

Mwandishi wa Radio Tehran mjini Mombasa, ametutayarishia ripoti hii hapa chini

Walimwengu wamepokea vizuri tangazao la Wakala wa Kimataifa wa Nisahti ya Atomiki IAEA kuhusu kufungamana Iran na ahadi zake katika mapatano ya nyuklia sambamba na taarifa ya pamoja ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na vilevile kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia yanayokwenda sambamba na kuondolewa vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kuondolewa vikwazo Iran ni ushindi kwa taifa hili ambalo lilisimama kidete katika kipindi chote cha mazungumzo hayo na kundi la 5+1. Salum Bendera amezungumza na Dakta Ahmad Khatib msomi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Dar es Salaam Tanzania na katika mahojiano hayo yaliyopo hapa chini anaanza kutoa tathmnini yake kuhusiana na kuanza kutekelezwa makubaliano hayo ya nyuklia...

Bomoabomoa ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya awamu ya tano jijini Dar es Salaam, Tanzania imekosolewa vikali na pande mbalimbali wakiwamo wananchi. Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi hao kutolipwa gharama na serikali kabla ya kutekelezwa operesheni hiyo suala ambalo limewaacha watu wengi katika hali mbaya ya kimaisha wakishindwa mahala pa kwenda kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa. Ili kujadili suala hilo Redio Tehran imezungumza na mbunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Maulid Mtulia ambaye naye amekosoa operesheni hizo kama ifuatavyo……….bonyeza chini upate sauti ya mahojiano hayo./

Mgogoro wa Burundi umeendelea kutokota licha ya jamii ya kimataifa kushinikiza pande hasimu nchini humo kutanzua tofauti baina yao kwa njia za amani. Hayo yamekuja baada ya serikali ya Burundi kutangaza azma yake ya kutowatuma wawakilishi wake kwenye mazungumzo huko mjini Arusha Tanzania kwa kile ilichokisema kuwa ni kujadili pamoja na magaidi. Wakati hayo yakijiri Adolphe Manirakiza, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Bujumbura ametoa pendekezo la kutaka kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa watuhumiwa wa mapinduzi yaliyofeli mwezi Mei mwaka jana 2015. Ili kujadili masuala hayo kwa ujumla tumezungumza na Rajabu Minani, mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa nchini Burundi ambaye ameanza kutoa tathmini yake kuhusiana na mgogoro huo……… bofya kwa chini upate sauti…../

Mkutano wa 29 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ambao ulifanyika hivi karibuni hapa mjini Tehran ulihudhuriwa na wasomi, wanazuoni na wanafikra zaidi ya 600 kutoka nchi 70 duniani. Mkutano huo ambao ulifanyika kwa mnasaba wa Maulidi ya Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu, ulikuwa na kaulimbiu  isemayo: "Migogoro ya Sasa Katika Ulimwengu wa Kiislamu". Mwenzetu Mubarak Henia alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wanazuoni na wageni wengine waliohudhuria kikao hicho, kutoka kanda ya Afrika Mashariki, akiwemo Sheikh Thabit Noman Jongo, Mkuu wa Fatwa na Utafiti katika Ofisi ya Mufti wa Zanzibar na hapa anaanza kwa kumuuliza……

Bonyeza hapa chini kuyasikiliza mahojiano hayo......

Ulimwengu wa Kiislamu unaomboleza kifo cha mwanachuoni na mwanaharakati mashuhuri wa Kiislamu nchini Saudi Arabia, Sheikh Nimr Baqir al-Nimr, ambaye ameuawa shahidi kwa kunyongwa na utawala wa Aal-Saud. Asasi za kiraia, watetezi wa haki wa binadamu na jamii ya kimataifa ya ujumla zimelaani ukatili huo wa serikali ya Riyadh. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imetangaza kuwa, hii leo imewanyonga watu 47 akiwemo Sheikh al-Nimr,  eti baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika operesheni za kigaidi. Sheikh Baqir al Nimr alikamatwa na kufungwa jela na utawala wa kifalme wa Saudia mwaka 2012 akiwa katika maandamano ya kupinga dhulma za utawala huo katika eneo la Qatif lenye idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. Mahakama Kuu ya Saudi Arabia ilikuwa imepasisha hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama moja ya nchi hiyo dhidi ya msomi huyo na utekelezaji wake ulikuwa ukisubiri saini ya Mfalme Salman bin Abdulaziz. Tumezungumza na msomi na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu, Sheikh Ally Ammar Mwazoa wa Tanga Tanzania, ambaye anaanza kwa kutoa tathmini yake kuhusiana na tukio hilo chungu la kuuawa wanaharakati wa Kiislamu….

 

Waislamu nchini Uganda wametakiwa kutojiingiza katika sherehe zisizokuwa za dini yao licha ya kwamba ni wajibu kuwaheshimu wafuasi wa dini nyinginezo katika sherehe na ibada zao.

Mwito huo umetolewa na Sheikh Shiwuyo wa Msikiti Mkuu wa Old Kampala nchini Uganda.

Mwandishi wa Radio Tehran amemuhoji Sheikh Shiwuyo na kuandalia ripoti ifuatayo: 

Wawakilishi wa wawasi pamoja na wa serikali ya Burundi wamekutana mjini Entebbe, karibu na Kampaka, mji mkuu wa Uganda chini ya upatanisi wa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo anayewakilisha Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC katika jitihada za kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Mwandishi wa Radio Tehran na maelezo zaidi...

Kamanda wa Jeshi la Uganda, Jenerali Katumba Wamala amewataka wananchi na wanasiasa wa nchi hiyo kuepuka machafuko na maneno yanayohatarisha amani katika kipindi hiki nyeti cha kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo na kuepusha kutumbukia nchi hiyo katika machafuko kama ya nchini Burundi.

Mwandishi wa Radio Tehran jijini Kampala na ripoti ifuatayo hapa chini:

Wakati hali ya kisiasa nchini Burundi ikiendelea kuwa tete, Viongozi wa Kiafrika wametakiwa kuacha kurudi nyuma badala yake wawe mstari wa mbele katika utatuzi wa mgogoro wa Burundi unaoendelea na kuacha kusubiri hali ya mambo nchini humo kuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Omar Manji na ripoti ifuatayo.