Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Na kufuatia kushadidi mvutano baina ya Burundi na Rwanda juu ya tuhuma kwamba serikali ya Kigali ilikuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Kirundi waliomo nchini humo, sasa serikali ya Bujumbura imetangaza azma yake ya kukaa kwenye meza moja ya mazungumzo na jirani yake huyo ili kumaliza switafahamu baina yao. Hayo yamedokezwa na Gaston Sindimwo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi ambaye pamoja na kauli yake hiyo ameendelea kuinyoshea kidole cha lawama Rwanda kupitia tuhuma zile zile za serikali yake kwamba, Kigali ni mchochezi na msababishi wa matatizo yanayoendelea nchini mwake. Ili kujadili suala hilo, tumezungumza na Rajabu Minani, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya kisiasa nchini Burundi na tumeanza kwa kumuuliza ……….bonyeza chini kupata sauti/

Mashirika ya kutetea haki za binaadamu nchini Kenye yamelaani na kutangaza kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa dhidi ya askari wawili waliohusika na mauaji ya mtoto mmoja nchini humo. Kwa mujibu wa hukumu hiyo, askari hao wamefungwa miaka saba, badala ya kifungo cha maisha.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa tarifa zaidi………../

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya IEBC leo Jumatatu imezindua mpango wa kuwasajili wapiga kura kutoka kile kona ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2017.  Tume hiyo imesema imeanza zoezi hilo mapema ili kuepusha manung’uniko kutoka kwa wadau mbali mbali na haswa viongozi wa upinzani nchini humo. Usajili huo wa wapiga kura wa nchi nzima unatazamiwa kuendelea hadi Machi 15.

Ili kupata tathmini kamili kuhusu hatua ya IEBC kuanza zoezi hilo mapema na changamoto zilizoko mbele yao kueleka uchaguzi mkuu mwakani, mwandishi wetu wa Nairobi Suleiman Yeri Ali amezungumza na Kamishna wa tume hiyo, Balozi Yusuf Nzibo…………………….

Wakati siku mia moja za rais mpya wa Tanzania  DK, John Pombe Magufuli madarakani zikitimia,Watanzania wamemtaka rais huyo kuongeza kasi ya kuwabana mafisadi wanaohujumu uchumi wa nchi hiyo bila kuwaonea huruma. Aidha raia wa nchi hiyo, wamemtaka Rais Magufuli kukuza uchumi sanjari na kutekeleza ahadi alizozitoa katika kampeni za uchaguzi uliopia, ambapo wamesema kuwa mengi ya aliyoyaahidi bado hajayatekeleza, ingawa amejitahidi kwa kiasi fulani.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Omar Manji kwa taarifa kamili….Bonyeza chini kupata sauti../

Mtandao wa WikiLeaks unaofichua siri za serikali mbalimbali duniani umefichuwa ripoti ya uvunjaji wa haki za binaadamu na udanganyifu wa Shirika la Uchimbaji madini ya Urani, AREVA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa mtandao huo, mbali na viongozi wa AREVA kujitajirisha kwa mabilioni ya Dola, wameihadaa serikali ya Bangui na hivyo kuikosesha serikali hiyo kiasi kikubwa cha pato lake kutoka kwa shirika hilo lenye miaka mingi nchini humo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati, Mosi Mwasi kwa taarifa kamili……………Bonyeza kupata sauti…./

Wataalamu wanawake wa Kiislamu nchini Kenya wamejitokeza na kulaani hatua ya kupewa likizo ya lazima afisa mkuu mtendaji wa shirika la mafuta nchini Kenya Sumaya Uthman na kumtaka Rais Uhuru Kenyatta na Waziri wa Kawi Charles Keter kumrejesha kazini mara moja.

Mwanahabari akiwa jijini Nairobi Suleiman Yeri Ali alikuwepo kwenye kikao hicho na kututayarishia ripoti hii

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewatoa hofu wananchi wa nchi hiyo akisema hakuna fujo zitakazotokea wakati au baada ya uchaguzi kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa. Kauli ya Museveni ni majibu kwa matamshi ya Jenerali David Sejusa aliyesema kuwa Uganda itateketea endapo kiongozi huyo atatumia hila kushinda katika uchaguzi ujao. Hivi sasa Jenerali Sejusa anashikiliwa katika jela ya Luzira.

Mwandishi wa Radio Tehran mjini Kampala ametutayarishia ripoti hii hapa chini

Baada ya Chama cha Wananchi CUF kutangaza kwamba hakitashiriki kwenye uchaguzi wa marudio uliopangawa kufanyika Machi 20 visiwani Zanzibar, wataalamu wa masuala ya siasa nchini Tanzania wanaona kuwa, kutopatikana ufumbuzi wa mvutano unaoendelea kati ya vyama vikuu vya siasa Zanzibar, kunaweza kusababisha hatari ya kuingia katika machafuko yatakayopelekea hali ya usalama kuwa hatarini visiwani Zanzibar.

Mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Tanzania ametutayarishia ripoti hii hapa chini.

Na baada ya kuuawa mtuhumiwa wa ugaidi Muhammad Mugemagango, aliyekuwa akiwapatia mafunzo ya ugaidi vijana wa Rwanda kwa lengo la kuwatuma nchini Syria kwenda kujiunga na makundi mengine ya kigaidi na kitakfiri kama vile Daesh, polisi ya nchi hiyo imetangaza kuwa imewatia mbaroni vijana wengine kadhaa ambao walikuwa na mafungamano na Bwana  Mugemagango jijini Kigali. Suala hilo limeibua hali ya wasi wasi kwa Waislamu wa nchi za eneo la Afrika ya Mashariki na Kati ambao wanauona Uwahabi kama chanzo kikuu cha ugaidi na ukatili duniani. Katika fremu hiyo, tumezungumza na Sheikh Jumanne Abdullah wa jijini Bujumbura, Burundi ambapo tumeanza kumuuliza chanzo cha vijana kuathiriwa na fikra hasi za Uwahabi zinazokinzana na Uislamu halisi wa Bwana Mtume Muhammad (saw), ambapo ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano hayo …………bonyeza chini kupata mahojiano hayo…./

Wakati Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar (ZEC) ikiendelea na maandalizi ya uchaguzi wa marudio visiwani humo utakaofanyika  hapo Machi 20 mwaka huu, chama cha wananchi CUF kimetoa tamko zito hapo jana kikipinga kurudi katika uchaguzi huo. CUF kimesisitiza kuwa, kinautambua tu uchaguzi uliopita wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana ambao ulitajwa na wasimamizi wa ndani na nje kuwa ulikuwa salama na usio na dosari yoyote.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Omar Manji kwa taarifa kamili……………Bonyeza chini kupata sauti…/