Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Mkuu wa Usalama wa Ndani wa nchini Kenya amelazimika kuwasimamisha kazi takriban maafisa wote wa usalama wa Wilaya ya Garissa kufuatia malalamiko makali ya taasisi mbalimbali za haki za binadamu, za kiraia na mirengo ya upinzani nchini humo.

Mashirika ya haki za binadamu ya Burkina Faso na Senegal yametishia kuzivamia balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo barani Afrika na barani Ulaya iwapo serikali ya Kinshasa haitowaachilia huru wanaharakati wa haki za binadamu wanaoshikiliwa nchini Kongo.

Mwandishi wa Radio Tehran amefuatilia suala hilo na kututayarishia ripoti ifuatayo

Baraza kuu la Ulamaa nchini Somalia liliketi wiki hii na kulaani rasmi mashambulio na mauaji yanayofanywa na kundi la kigaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo nchi jirani ya Kenya.

Vile vile baraza hilo limeitaka serikali ya Kenya iwalinde Waislamu na isitoe mwanya wa kutumiwa vibaya mashambulio ya kigaidi ya ash Shabab kukandamizwa Waislamu wasio na hatia.

Hayo na mengine yamo katika ripoti ya juma moja ya Kiislamu iliyoandaliwa na mwandishi wa Zanzibar Hassan Issa Ali.

Ingia hapa chini kusikiliza ripoti hiyo.

Sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatwimat Zahraa (as), binti ya Mtume Muhammad (saw), wanawake duniani wametakiwa kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwazuia wasiweze kurubuniwa katika kujiunga na makundi ya kigaidi na kitakfiri. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Nairobi, Murtadhaa Shafii Shakiib ambapo pia amewaasa kwa mambo mengi.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Nairobi Hussein Hassan kwa taarifa zaidi...

Serikali ya Tanzania imelazimika kutengua uamzi wake wa kutaka madereva wa mabasi ya abiria nchini humo, kurudi mafunzoni kila baada ya miaka mitatu, baada ya madereva hao kufanya mgomo wa kutoa huduma za usafirishaji nchi nzima. Katika mgomo huo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutuliza ghasia zilizosababishwa na madereva hao.
Mwandishi wetu Grayson Gideon na taarifa zaidi kutoka Dar es Salaam

Mauaji ya kutisha yaliyoenea magharibi mwa dunia hadi mashariki yake, na kaskazini mwa sayari hii hadi kusini mwake, yanasababishwa na nini hasa? Habari zinasema kuwa, aliyeongoza mauaji ya halaiki huko Garissa nchini Kenya alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu, hali ni hiyo hiyo kwa baadhi ya wafuasi wa makundi ya kigaidi kama vile Boko Haram, Daesh, Jabhatunnusra na mengineyo! Hii fikra hii ya kuamua kuvamia na kuua watu bila ya kuwa na hisia za kibinadamu inatokana na nini hasa kutokana na kwamba inavyotarajiwa msomi wa Chuo Kikuu tena awe mtu mwenye muono mpana, asiyetenda mambo kwa hasama zisizo na mantiki ndani yake? Swali hilo tumemuuliza Sheikh Juma Ngao, Mwenyekiti wa taasisi ya KEMNAC ya nchi Kenya na alikuwa na haya ya kusema:

Wananchi visiwani Zanzibar wametakiwa kuwaenzi viongozi wao kutokana na juhudi za viongozi hao walizozifanya kuhakikisha wanafikia hapo walipo. Hayo yameelezwa leo ikiwa ni katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mzee Karume, mwasisi wa Zanzibar, kumbukumbu ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali ya visiwa hivyo.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Grayson Gideon kwa taarifa zaidi...

Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yameendelea kusisitiza juu ya kufanyika uchunguzi wa haraka kufuatia kugunduliwa kaburi moja la halaiki karibu na Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa baadhi ya duru, wahanga wa mauaji hayo, waliuawa katika maandamano ya mwezi Januari mwaka huu.
Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi kwa taarifa zaidi

Maziko ya Mkuu wa chama cha NRA cha nchini Tanzania, Rashid Hashim Mtuta yalifanyika kwa kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemo shakhsia mbalimbali wa kisiasa na kidini wa nchi hiyo.

Mwanasiasa maarufu, Profesa Kigoma Malima, aliwahi kuwa mkuu wa chama hicho. Bwana Rashid aliwahi pia kuwa mjumbe katika lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba nchini Tanzania.

Mwandishi wa Radio Tehran alishiriki kwenye maziko hayo na kutuandalia ripoti ifuatayo.

Wananchi wa Kenya wamefanya maandamano jijini Nairobi kulaani shambulio la kigaidi dhidi ya Chuo Kikuu cha Garissa lililouwa watu wapatao 150, Alkhamisi iliyopita. Maandamano hayo yamefanyika katika siku ya mwisho ya maombolezo ya kitaifa ambapo bendera zilipepea nusu mlingoti.
Mwandishi wetu wa Nairobi Hussein Hassan ana maelezo zaidi