Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Kwa mara nyingine tena viongozi wa Kiislamu nchini Kenya wameeleza hofu yao kutokana na kukithiri kwa visa vya kuuawa na kutoweka kwa wakaazi wa maeneo ya Kaskazini Mashariki katika mazingira ya kutatanisha.
Wakaazi wa kaunti zilizoko katika maeneo hayo wanahisi kuwa wimbi hilo la mauaji na ukandamizaji linaendelezwa na vyombo vya usalama nchini humo vikidai ni vita dhidi ya ugaidi.
Mwandishi wetu wa Nairobi ametutumia taarifa ifuatayo.....

Msemaji wa Rais Pierre Nkurunzinza ameiambia Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran kuwa uchaguzi mkuu wa Burundi utaendelea kama ulivyopangwa na kwamba zoezi hilo halitoakhirishwa. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Gervais Abayeho amesema wagombea 8 wa kiti cha urais tayari wamewasilisha makaratasi yao akiwemo Rais Pierre Nkurunziza. Msemaji wa Rais pia amelaani jaribio la mapinduzi lililofeli na kuthibitisha kuwa majenerali kadhaa wa jeshi walioendesha jaribio hilo wametiwa mbaroni.

Sikiliza mahojiano na Bw. Abayeho kupitia RealPlayer hapa chini

 

Huku serikali ya Kenya ikiendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na visa vya ugaidi, suala la ufisadi pia limeendelea kuwa gumzo miongoni mwa Wakenya wa kada mbalimbali. Wanasiasa, viongozi wa asasi za kiraia na wale wa kidini wamepongeza hatua ya serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ya kuwasimamisha kazi maafisa wanaojihusisha na ulaji rushwa ingawa kambi ya upinzani imesisitiza kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya Rais Kenyatta ni za kimaonyesho na sarakasi ya kisiasa.

Salim Swaleh amepata fursa ya kukutana na kuzungumza na mbunge kutoka chama cha upinzani cha ODM, Mhe. Samuel Arama na haya hapa mahojiano hayo maalumu

Bajeti ya Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini Burundi imekumbwa na nakisi ya asilimia 80. Hayo ni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Burundi.
Hali hiyo imejitokeza baada ya Ubelgiji na Umoja wa Ulaya kusisimamisha msaada wa euro milioni 4 za kuendeshea uchaguzi huo baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea tena urais kwa muhula wa tatu mfululizo.
Wakati huo huo maandamano ya kupinga hatua hiyo ya Rais Nkurunziza yanaendelea. Watu wengine watatu wameuawa kwenye maandamano ya karibuni kabisa.

Mwandishi wa Radio Tehran na ripoti ifuatayo

Jumatano, 13 Mei 2015 12:59

Madhara ya mafuriko nchini Tanzania

Mvua zilizonyesha kwa wingi nchini Tanzania zimesababisha madhara makubwa vikiwemo vifo na mamia ya familia kupoteza maisha yao.


Vitu vingi vya thamani vimeharibiwa na mvua hizo hususan jijini Dar es Salaam.


Barabara nyingi zililazimika kufungwa kwa muda katika baadhi ya maeneo.

Hapa chini tumekuwekeeni moja ya ripoti za mwandishi wetu wa Dar es Salaam.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema iko tayari kuisaidia Kenya katika juhudi zake za kupambana na kundi la wanamgambo wa Ashabaab la Somalia pamoja na kuzima wimbi la vijana kushawishiwa kujiunga na makundi yenye misimamo mikali.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Iran nchini humo Malek Hossein Givzad, ambaye pia ameitaka jamii ya kimataifa kutofumbia macho jinai wanazofanyiwa wananchi wasio na hatia wa Yemen.

Mwandishi wetu Hussein Hassan ana maelezo zaidi kutoka Nairobi

Ubelgiji imechukuwa hatua ya kusimamisha msaada wake wa euro milioni mbili kwa ajili ya uchaguzi wa Burundi.


Hatua kama hiyo imechukuliwa pia na Umoja wa Ulaya Ulokuwa uipatie Burundi milioni nyingine mbili za kugahrimu uchaguzi.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.

Mwandishi wetu wa Burundi na ripoti zaidi. 

Baadhi ya wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchini Rwanda wameiomba serikali ya Burundi kukomesha vitendo vya usalama mdogo vinavyoendeshwa na vijana wanaoegemea chama tawala cha CNDD-FDD maarufu kama Imbonerakure.
Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi

Viongozi mbalimbali na wananchi wa Kenya wamejitokeza kulaani hatua ya mahakama ya kilele ya nchi hiyo ya kuruhusu kusajiliwa chama cha ulawiti na usagaji nchini humo. Wakenya wameipa serikali muda wa hadi wiki ijayo kubadilisha uamuzi huo.
Mwandishi wetu Seifullah Murtadha na ripoti zaidi kutoka Mombasa, Kenya.

Jumatano, 29 Aprili 2015 15:34

Mahojiano kuhusiana na hali ya mambo Burundi

Na kama mlivyosikia katika taarifa yetu ya habari kwamba machafuko nchini Burundi yameendelea kwa siku ya tatu mtawalia ambapo wananchi wanapinga hatua ya chama tawala nchini humo, kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kugombea katika uchaguzi ujao ambapo wanaitaja hatua hiyo kuwa ni kupingana na katiba ya nchi hiyo. ili kujadili zaidi suala hilo, tumezungumza na Rajabu Minane, mwandishi wa habari wa jijini Bujumbura ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa, ambapo ameanza kuelezea kile kinachojiri nchini humomo hivi sasa…./