Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili

Mshauri wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Willy Nyamitwe amesema kuwa, hadi sasa bado serikali ya nchi hiyo haijapata mwaliko wa kuhudhuria mazungumzo ya kisiasa yaliyoitishwa na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa hapo tarehe Pili hadi sita mjini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo ya Tanzania. Hayo yanajiri katika hali ambayo mauaji ya kuvizia nchini Burundi yameendelea kushuhudiwa dhidi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa kamili…………………/

Hofu ya kusambaa kwa maradhi ya Hepatitis A imeukumba mji wa Mombasa nchini Kenya huku mikakati ikiwekwa na serikali ili kudhibiti kusambaa kwa maradhi hayo. Katika fremu hiyo, viongozi wa afya wamekuwa wakiendesha zoezi la kuweka madawa ya kuzuia maambukizi ndani ya visima vya maji ndani ya jiji hilo la Mombasa.

Mwandishi wetu Seifullah Murtadha ametuandalia taarifa ifuatayo……………………………../

Mataifa 11 ya Kiafrika yamekubaliana kuweka viwango sawa vya matumizi ya simu ili kuwarahisishia raia wa mataifa hayo. Taarifa iliyotolewa na nchi hiyo, imesema kuwa, mataifa hayo yamefanikiwa kupata mafanikio makubwa punde tu baada ya kuanzishwa mfumo huo ndani ya mataifa ya Kenya, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi……………………/

Nchini Kenya vitendo vya mauaji dhidi ya shakhsia wa kidini vilivyokithiri ndani ya taifa hilo, huenda vikapata dawa yake baada ya mahakama kuu kuanza kutoa hukumu kali kwa wahusika. Hatua hiyo imekuja baada ya jaji wa mahakama kuu nchini Kenya kutoa hukumu ya adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa mmoja wa washukiwa wa mauwaji ya Sheikh Muhammad Idriss aliyekuwa Mkuu wa Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini Kenya CIPK. 

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa taarifa kamili……………/

Serikali ya Tanzania imeshutumiwa kwa kuulemaza umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC katika kuyafikia malengo tarajiwa. Hayo yamesemwa na wabunge wa jumuiya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine wameitaja Tanzania kuwa inakhofia kuingia katika ushindani wan chi wanachama katika jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa Seifullah Murtadha kwa taarifa zaidi………

bonyeza hapa chini kusikia sauti.........../ 

Huku Umoja wa Mataifa ukisisitizia umuhimu wa kuchukuliwa adhabu kali kwa askari wa umoja huo wanaosimamia amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na kuhusika na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo na wanawake, inaonekana sisitizo hilo halijawaathiri askari hao. Hayo yamekuja baada ya kamanda mmoja wa Ufaransa kuhusishwa na jinai mpya mbaya ya ukatili wa kijinsia ambapo mbali na kuwabaka mabinti wadogo wanne aliwaamuru pia watoto hao kufanya ufuska na mbwa wake, kitendo ambacho kimepelekea mmoja wa watoto hao kufariki dunia. Mwandishi wetu wa eneo la Afrika Mosi Mwasi na anaelezea tukio hilo la kusikitisha. Pata sauti kamili......

Wito wa umoja, mshikamano na kuwa na misimamo ya wastani miongoni mwa Waislamu umetolewa mwishoni mwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Waislamu zaidi ya elfu 6 aghalabu yao wakiwa vijana walihudhuria duru ya tatu ya kongamano hilo la kila mwaka linalojukana kama ‘Journey of Faith’ lililofanyika katika Jumba la KICC na kumaliza shughuli zake Jumatatu ya jana ya Machi 28. Mbali na viongozi wa kidini, kisiasa na kijamii wa Kenya, wanazuoni na wanafikra kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo Canada, Uingereza na Marekani wamewasilisha mada tofauti katika kongamano hilo. Tumezungumza na Sheikh Yusuf Abdu, msomi wa Kiislamu, mwanaharakati na mshairi kutoka Mombasa, ambaye ni mmoja wa wanazuoni waliyohutubia kongamano hilo.....

 

 

Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, FaustinArchange Touadera ameanza kufuata hatua zilizochukuliwa na Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania katika kubana matumizi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi. Hatua hiyo imekuja baada ya rais huyo kupiga marufuku ya sherehe ambazo zingefanyika siku ya kuapishwa kwake kuchukua mikoba ya Rais wa sasa Bi Cathirine Samba Panza.

Ili kujadili suala hilo tumezungumza na Mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi na tulianza kwa kumuuliza……./

Polisi nchini Uganda imeendelea kumzuilia nyumbani, Dakta Kiza Besigye, licha ya kumalizika zoezi la uchaguzi uliompa ushindi Rais Yoweri Museven wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa polisi hiyo, hatua hiyo inafanyika kwa lengo la kumzuia mwanasiasa huyo wa upinzani ili asiweze kuibua fujo kama ambazo zimekuwa zikitokea katika mataifa mengine ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Kampala, Kigozi Islamail kwa taarifa kamili……Bonyeza chini kupata sauti../

Mkutano wa hivi punde wa nchi ambazo zina polisi na askari wake nchini Somalia chini ya mwavuli wa AMISOM, umetoa wito wa kutumwa askari zaidi wa nchi za Afrika kujiunga na kikosi hicho. Mkutano huo wa Djibouti umefanyika mwezi mmoja baada ya makumi ya askari wa Kenya KDF kuviziwa na kuuawa na wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabab katika kambi ya El-Adde. Licha ya magaidi hao kudai kuwa waliua zaidi ya askari 100 wa Kenya, lakini serikali ya Nairobi mpaka sasa haijasema chochote kuhusu idadi ya wanajeshi wake waliouawa. Kwa sasa, Kenya, Uganda, Burundi, Djibouti na Ethiopia ndizo nchi pekee zilizotuma wanajeshi wake nchini Somalia, chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM. Ili kujadili kadhia hiyo, tumezungumza na Bwana Simiyu Werunga, mchambuzi wa masuala ya usalama kutoka Nairobi Kenya, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya African Centre on Security and Strategic Centre…….  

Page 1 of 37