Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 20 Machi 2016 11:49

1395 H/Shamsia mwaka wa uchumi wa kimuqawama

1395 H/Shamsia mwaka wa uchumi wa kimuqawama

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuanza kwa mwaka mpya 1395 Hijiria Shamsia na kutoa mkono wa kheri na fanaka kwa sikukuu hii ya Nairuzi kwa wananchi wote wa Iran. Katika ujumbe huo, Kiongozi Muadhamu ameutaja mwaka huu kuwa ni mwaka wa 'Uchumi wa Kimuqama, Hatua na Vitendo'

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameashiria kuwadia tarehe ya kuzaliwa Bibi Fatwimat Zahra (as) binti wa Bwana Mtume Muhammad (saw) mwanzoni mwa mwaka huu mpya na kuelezea matarajio yake kwamba mwaka huu wa 1395 utakuwa wenye mafanikio kwa taifa la Iran na taifa hili litaweza kustafidi na umaanawi wa bibi huyo mtukufu kupitia darsa za miongozo yake pamoja na maisha yake. Aidha Kiongozi Muadhamu amesema mwaka uliomalizika wa 1394 Hijiria Shamsia kama ilivyokuwa miaka mingine nao ulikuwa na 'matamu na machungu' 'milima na mabonde' na 'fursa na vitisho.' Amesema kuwa, tukio chungu kabisa katika mwaka uliopita, lilikuwa ni maafa ya mahujaji eneo la Mina nchini Saudia, ambapo maelfu ya mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu walipoteza maisha katika tukio hilo la kuumiza, huku utamu wake ukiwa ni 'maandamano ya wananchi wa Iran ya tarehe 22 Bahman na pia uchaguzi wa tarehe saba Isfand.' Aidha amekutaja kutiwa saini makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) baina ya Iran na madola sita yenye nguvu zaidi duniani, makubaliano ambayo yaliandamana na matumaini katika sehemu moja na wasi wasi kwa upande wa pili kuwa ni matukio mengine muhimu yaliyiokuwemo katika mwaka huo. Ameashiria matumaini, fursa na vitisho katika mwaka huu mpya na kusisitiza kuwa, jambo bora ni kutumia kwa maana halisi fursa zinazojitokeza na kuvigeuza vitisho kuwa fursa, kiasi kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka, kuweze kuonekana tofauti za wazi baina ya mwaka huu na miaka mingine. Amesema kuwa katika kufikiwa hayo kunahitajika juhudi, utendajikazi wa usiku na mchana na kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)