Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 27 Februari 2016 20:18

Kiongozi Muadhamu ataka kuimarishwa uhusiano wa Iran na Uswisi

Kiongozi Muadhamu ataka kuimarishwa uhusiano wa Iran na Uswisi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa historia ya Uswisi ya kutojiunga na mashinikizo na vikwazo vya baadhi ya nchi za Magharibi dhidi ya Iran ni miongoni mwa nyanja nzuri za kiutamaduni kwa ajili ya kuzidisha ushirikiano wa pande hizo mbili.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi aliyeko safarini hapa nchini. Ameashiria historia ya uhusiano wa nchi mbili hizi na taswira nzuri ya mwenendo wa serikali ya Uswisi katika fikra za Wairani na kukaribisha suala la kustawishwa zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kielimu wa pande mbili.

Ameashiria pia tajiriba ya wananchi wa Iran kuhusu hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kuchochea vita ikiwa ni pamoja na kuupatia utawala wa Saddam Hussein makombora na ndege za kivita wakati wa vita vilivyoanzishwa na utawala huo dhidi ya Iran na akasema: Mwenendo huo umejenga taswira hasi katika fikra za wananchi wa Iran lakini taswira kama hiyo haiko hapa nchini kuhusu Uswisi.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono kikamilifu mahusiano ya kiuchumi na dhamana ya kisheria ya makubaliano ya Iran na Uswisi na kuongeza kuwa, jambo muhimu ni kuona makubaliano hayo yakitekelezwa kivitendo kwa ushirikiano halisi, azma na irada thabiti.

Kwa upande wake Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi ameeleza kufurahishwa kwake na safari yake hapa nchini na kuashiria historia ya miaka mingi ya uhusiano wa kirafiki wa nchi yake na Iran. Amesema kuwa katika safari yake mjini Tehran kumejadiliwa ramani ya njia ya ushirikiano mpana zaidi na wa nyanja mbalimbali kati ya Iran na Uswsi na kwamba, kutiwa saini ramani hiyo ya njia kunaweza kupeleka kupanuliwa zaidi uhusiano wa pande mbili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)