Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 03 Februari 2016 17:42

"Baraza Kuu la Usalama wa Taifa linapaswa kutawaliwa na mantiki na fikra sahihi"

 "Baraza Kuu la Usalama wa Taifa linapaswa kutawaliwa na mantiki na fikra sahihi"

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa anga inayotawala sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na maamuzi yake inapaswa kwenda sambamba na fikra sahihi, halisi za kimapinduzi na za kihizbullah.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo katika hadhara ya viongozi wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na wataalamu wa sekretarieti ya baraza hilo waliokwenda kukutana naye. Ameashiria utata unaohusiana na suala la 'usalama' katika dunia ya sasa na kusema: Usalama ni haja muhimu sana kwa jamii na kwa msingi huo suala hilo limeashiriwa mara nyingi katika Qur'ani Tukufu. Amesisitiza kuwa, suala la usalama katika dunia ya sasa limevuka mzingo wa masuala ya kijeshi na kugusa pia masuala ya uchumi, maisha, utamaduni, siasa, kijamii, fikra na maadili.

Ayatullah Khamenei amesema wadhifa wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa ni kuwa na mtazamo kamili na mpana kuhusu suala la usalama na kutilia maanani pande zake zote.

Ayatullah Khamenei ameashiria njama za baadhi ya watu za kutaka kubadili misingi mikuu na ya wazi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kuwa: Imam Khomeini ni dhihirisho la Mapinduzi ya Kiislamu na kwa msingi huo hotuba zake zilizoandikwa katika makumu ya vitabu ni misingi ya Mapinduzi.

Amesema kuwa tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini baadhi ya watu hawakukubaliana na fikra za kimapinduzi na baadhi yao pia hawakuwa na itikadi ya kupambana dhidi ya ubeberu licha ya kuwa ndani ya mfumo wa Kiislamu; hivyo kuna udharura wa kukabiliana na mrengo huu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa katika kipindi chote cha miaka 37 iliyopita ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini daima kumekuwepo mapambano na kuongeza kuwa, hii leo mpambano huo umekuwa mgumu na tata sana kutokana na mbinu mpya na tata zinazotumiwa na adui kama maudhui ya anga ya intaneti na taathira zake za kiutamaduni, kiitikadi, kijamii na dhidi ya usalama.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)