Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 31 Januari 2016 17:47

Kiongozi Muadhamu awapa nishani ya ushindi makamanda wa Iran waliowakamata wanajeshi wa Marekani

Kiongozi Muadhamu awapa nishani ya ushindi makamanda wa Iran waliowakamata wanajeshi wa Marekani
Makamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH wamepewa nishani ya ushindi na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na makamanda hao kuwakamata wanajeshi wa Marekani walioingia katika maji ya Iran kinyume cha sheria.

Admirali Ali Fadavi, Kamanda wa Jeshi la Majini la Sepah na makamanda wengine wanne wa jeshi hilo, waliongoza operesheni ya kishujaa ya kusimamisha na kuzikamata boti mbili za Marekani na wanajeshi kumi waliokuwemo ndani yake katika eneo la kisiwa cha Farsi cha kusini mwa Iran. Makamanda hao wa jeshi la Sepah wamepata nishani hiyo ya ushindi kutokana na operesheni yao hiyo ya kishujaa iliyofanywa haraka sana mara baada ya wanajeshi hao wa Marekani kuingia katika maji ya Iran tarehe 12 mwezi huu wa Januari kinyume cha sheria.

Aidha Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amekubaliana na suala la kupandishwa cheo makamanda na maafisa wengine wa jeshi hilo walioshiriki katika operesheni hiyo kama ilivyopendekezwa na komandi kuu ya vikosi vya ulinzi nchini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)