Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Januari 2016 06:46

'Azma ya kweli ndiyo njia ya kufelisha njama za adui'

'Azma ya kweli ndiyo njia ya kufelisha njama za adui'

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya barani Ulaya na kusema kwamba, kuwa na nia na azma ya kweli na kufanya jitihada zilizosita vijana wote na wanachuo wa Iran ndiyo njia pekee ya kufelishda njama za kambi ya adui iliyosimama kukabiliana na Iran ya Kiislamu.

Matini ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu iliyosomwa jana Ijumaa na Hujjatul Islam Walmuslimin Javad Ejei, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika masuala ya wanachuo wa barani Ulaya kwenye kikao cha 50 cha kila mwaka cha umoja huo kilichofanyika mjini Milan, Italia ni kama ifuatavyo:

 

Bismillahir Rahmanir Rahim

Kwa vijana wapendwa

Hivi sasa umoja wenu umetimiza miaka khamsini na umoja huo ni chombo kilichobarikiwa ambacho kimeunganisha pamoja uongofu wa Kiislamu na shauku na unyofu wa imani na kujipamba kwa sifa za ujana na uanachuo na matunda yake yanaweza kuwa ni kuzaa watu wasomi, wenye hekima, wanaomcha Mwenyezi Mungu na wenye muono wa mbali.

Fanyeni jitihada za kuhakikisha kuwa mnajioanisha kadiri mnavyoweza - nyinyi na umoja wenu - na malengo hayo makubwa na yenye kuleta ufanisi.

Nchi na taifa lenu linakuhitajieni watu kama nyinyi katika jitihada zake za kuvuka njia hii ndefu. Nia ya kweli na jitihada zenu zisizosita na za vijana na wanachuo wote wa Iran ni muhimu mno katika juhudi za kuzifelisha na kuzifanya tasa njama zote za kambi ya adui iliyosimama kukakabiliana na Iran ya Kiislamu iliyojaa fakhari, kambi ambayo inatumia silaha za kila namna kuendeshea njama zake hizo. Nyoyo zenu zilizojaa matumaini na uwezo wenu uliojaa nguvu za kimaada na kimaanawi ziwekeni tayari tayari wakati wote na zidini kusonga mbele kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, Mweledi na Mwingi wa hekima.

Mwenyezi Mungu akulindeni na akusaidieni.

Sayyid Ali Khamenei

Dei 28, 1394

(Januari 18, 2016).

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)