Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 13 Januari 2016 17:33

Kiongozi Muadhamu: Wanavyuoni wajihusishe na sanaa

Kiongozi Muadhamu: Wanavyuoni wajihusishe na sanaa
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, dini tukufu ya Kiislamu si tu kwamba inaunga mkono masuala ya sanaa, lakini hata inashajiisha kufanya kazi za kisanii.

Amesema hayo wakati alipoonana na wasimamiaji na waendeshaji wa Kongamano la Taifa la Fikihi ya Sanaa na kuongeza kuwa, mifano mingi ya sanaa katika historia ya Uislamu ni uthibitisho wa namna dini hiyo ya Mwenyezi Mungu inavyolipa umuhimu suala la sanaa.

Ayatullah Khamenei ameashiria namna sanaa ilivyokita mizizi katika jamii za mwanadamu leo hii na athari zake za moja kwa moja katika fikra, roho na mtindo wa maisha ya watu na kutaja mambo ya lazima ya wanavyuoni wa fikihi katika suala zima la kutoa fatwa kuhusiana na kazi za sanaa. Amesema, inabidi usuli na misingi ya fikihi ichungwe kikamilifu na kutolewe fatwa kwa kutegemea Qur’ani na Sunna, bila ya kuathiriwa na wimbi na anga inayotawala katika jamii.

Vile vile amesema, kati ya wanavyuoni na mafakihi wa hawza (vyuo vikuu vya kidini) kumejaa watu waliobobea katika sanaa na ambao ni majimbi katika bahari za tungo na fasihi, hivyo ni muhimu kwa wanavyuoni wa kidini kutumia vizuri sanaa kutangaza Uislamu sahihi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)