Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 09 Januari 2016 16:44

Kiongozi: Mapinduzi ya Kiislamu yanazidi kuimarika

Kiongozi: Mapinduzi ya Kiislamu yanazidi kuimarika

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, licha ya kuweko mashinikizo yote haya dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, lakini yameendelea kuwa imara kwenye misingi na malengo yake matukufu ya tangu awali.

Ayatullah Khamenei amesema hayo leo wakati alipoonana na maelfu ya maulamaa na wananchi wa Qum na huku akiwapongeza wananchi wa Qum kwa mapambano yao ya Dei 19 (ya mwezi Januari 1976) ya kuunga mkono viongozi wa kidini ameelezea sababu zinazopelekea kuzidi kuwa imara Mapinduzi ya Kiislamu akisema: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameendelea kuwa imara na kuliletea utulivu taifa na kuzishinda njama zote za maadui kutokana na mwamko na kuwa macho wananchi na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei aidha amesema: Baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2009 nchini Iran, Wamarekani waliamua kujaribisha mbinu waliyoifanya na kufanikiwa katika baadhi ya nchi, ya kuchochoea machafuko kwa kisingizio cha uchaguzi nchini Iran, hivyo waliwakuza sana watu wachache ambao walikataliwa na wananchi katika kura, kwa kuwasaidia kifedha na kisiasa ili kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo, lakini Mapinduzi ya Kiislamu yalifelisha mapinduzi yao ya "rangi" nchini Iran kwa uungaji mkono kamili wa wananchi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mwito kwa wananchi wa Iran kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi ujao wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na ule wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu na kusema kuwa, kujitokeza kwa wingi wananchi kwenye chaguzi hizo kutazidi kuutia nguvu na kuuimarisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, na kutaendelea kudhaminiwa usalama kamili wa nchi, kuongezeka heshima na itibari ya taifa la Iran mbele ya walimwengu na kutapandisha juu haiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya maadui.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)