Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 05 Januari 2016 19:30

Kiongozi: Matatizo ya Afghanistan yatatuliwe kwa umoja

Kiongozi: Matatizo ya Afghanistan yatatuliwe kwa umoja

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa njia ya kutatua matatizo ya Afghanistan ni muungano wa kaumu na umoja wa viongozi wa nchi hiyo.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Abdullah Abdullah, Rais Mtendaji wa serikali Afghanistan. Kiongozi Muadhamu ameashiria historia na uwezo wa ushirikiano wa Iran na Afghanistan kuongeza kuwa, "Usalama, utulivu na ustawi wa Afghanistan" ni usalama na ustawi wa Iran.

Ayatullah Khamenei amekumbusha uungaji mkono wa Iran kwa taifa la Afghanistan kama upinzani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya hatua ya Shirikisho la Sovieti kukalia kwa mabavu nchi hiyo na kusema Iran iliwaunga mkono mujahidina wa Afghanistan na hivi sasa pia inaiunga mkono Afghanistan kwa kuwapa hifadhi raia milioni tatu wa nchi hiyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria suala la kuwepo wanafunzi elfu 16 Waafghani nchini huku wengine wengi pia wakiwa wameshahitimu katika vyuo vya hapa Iran na kusema hii ni fursa kwa wananchi wa Afghanistan. Ameongeza kuwa, serikali ya Afganistan inapaswa kuwapa vishawishi raia wake waliohitimu masomo Iran ili waweze kurejea nyumbani na kuihudumia nchi yao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kupanuka kiwango cha ushirikiano wa Iran na Afghanistan ni kwa maslahi ya nchi hizi mbili na kwamba baadhi ya hitilafu zilizopo kama zile zinazohusu maji ya mpakani zinapaswa kutatuliwa kwa urafiki na maelewano.

Aidha Kiongozi Muadhamu amekosoa sera za kuwatenga mujahidina wa Afghanistan katika miaka ya hivi karibuni na kusema: "Kuwatenga mujahidina kwa kuwapachika majina kama vile 'mababe wa kivita' ni siasa ghalati na katika nchi ambayo inakabiliwa na hatari ya hujuma ya kijeshi na fitina, wananchi wanapaswa kuwa na moyo wa jihadi na wawe tayari kulinda nchi yao.

Ayatullah Khamenei ameashiria mauaji yanayofanywa na Marekani nchini Afghanistan sambamba na kuisababishia nchi hiyo hasara kubwa na kuongeza kuwa, "Wamarekani bado wanaisakama Afghansitan lakini kutokana na kukita mizizi moyo wa mapambano baina ya watu wa Afghanistan na kushikamana kwao na dini, jambo ambalo ni maarufu katika historia, hakuna mvamizi na mkaliaji mabavu aliyewahi kufanikiwa Afghanistan.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)