Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 04 Januari 2016 18:29

'Maadui wanafanya njama za kuzuia fikra ya Kiislamu'

'Maadui wanafanya njama za kuzuia fikra ya Kiislamu'

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia haja ya kushiriki kwa wingi inavyowezekana wananchi wa Iran katika uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na uchaguzi wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu).

Ayatullah Khamenei amesema hayo leo asubuhi wakati alipoonana na Maimamu wa Sala za Ijumaa kutoka pembe zote za Iran. Ameongeza kuwa, chaguzi za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na Baraza la Wanavyuoni Wataalamu zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni ni muhimu na kusisitiza kuwa, katika upande wa ndani ya nchi, chaguzi hupelekea taifa kuhisi kuwa na uhuru na utambulisho na katika upande wa kieneo na kimataifa, uchaguzi unaipa heshima Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei amegusia pia namna Wamarekani wanavyouangalia kwa jicho la tamaa uchaguzi ujao humu nchini ili wakipata fursa yoyote waitumie kutekeleza njama zao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Wamarekani wanafanya njama za kuiweka mbali jamii ya Iran na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu ili Iran isikaribie kwenye malengo yake, lakini taifa kubwa na lililo macho la Iran huwa mara zote linafanya kinyume kabisa na anavyotamani adui, iwe ni katika uchaguzi au katika masuala mengineyo.

Ayatullah Khamenei amesema katika sehemu nyingine ya hotuba yake kuwa, kambi kubwa ya maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu na taifa la Iran wanatumia njama za kila namna kujaribu kuzuia kuenea aidiolojia na fikra za Uislamu sahihi katika maeneo tofauti kutokana na kuona maslahi yao yako hatarini.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, fikra ya Uislamu sahihi ni mithili ya upepo mwanana wenye harufu nzuri unaolea watu makini katika maeneo tofauti duniani, na ni kwa sababu hiyo ndio maana wapinzani wa Uislamu wanaishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kila aina ya mashambulizi ya kisiasa na kipropaganda ili kukabiliana na uhakika huo.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)