Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 01 Disemba 2015 19:40

'Mantiki ya Iran ni kuwa na uhusiano na mataifa yote '

'Mantiki ya Iran ni kuwa na uhusiano na mataifa yote '

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: 'Mantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kustawisha uhusiano na mataifa yote ya dunia."

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo mjini Tehran katika mazungumzo yake na Viktor Orban, Waziri Mkuu wa Hungary aliyekuwa safari hapa nchini

Kiongozi Muadhamu amebainisha kuwa taifa la Iran halina kumbukumbu yoyote mbaya kuhusu Hungary na kwa msingi huo itajibu sera za uaminifu kwa sera za ukweli. Ameashiria nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya Iran na Hungary na kusema, sera zilizotangazwa na serikali ya Hungary za 'Kuelekea Asia' ni sera sahihi na zinaweza kuwa chanzo cha kuimarishwa uhusiano.  Ayatullah Khamenei amesema chimbuko la uhasama na chuki nyingi ni kutokuwepo ufahamu sahihi baina ya pande mbili na kuongeza kuwa: "Leo katika mazingira ya kipropaganda yaliyopo duniani, ukweli unapotoshwa na hali hii ya mazingira yaliyochafuka ina madhara kwa wanadamu wote."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mazungumzo mazuri yaliyoanzishwa na Iran baina ya ulimwengu wa Kiislamu na Ukristo na kuongeza kuwa: "Kutumia fursa hizi kwa ajili ya kuimarisha nukta za pamoja na kuweka wazi ukweli ni hatua ya kujenga ufahamu sahihi ukiwemo ule unaohusiana na sheria za Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: 'Hivi sasa umaanawi na masuala ya kiroho yanaenea hatua kwa hatua Ulaya na Marekani ambapo vijana ni mhimili mkuu wa harakati hii na kwamba katika siku za usoni Ulaya inaweza kushuhudia mlingano baina ya ustawi wa kimaada, kisayansi na kiteknolojia pamoja na umaanawi na masuala ya kiroho.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, ameashiria udharura wa kuimarisha ushirikiano wa Iran na Hungary. Amesema kwa kuzingatia nafasi muhimu ya Iran kimataifa, kuna matumaini ya kutumia fursa zilizopo kuimarisha uhusiano wa pande mbili.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)