Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 21 Januari 2016 18:59

"Iran imetimiza malengo yake makuu katika mazungumzo ya nyuklia"

"Iran imetimiza malengo yake makuu katika mazungumzo ya nyuklia"

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran imefikia karibu malengo yake yote makuu baada ya kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kati ya Tehran na nchi zinazounda kundi la 5+1.

Rais Hassan Rouhani ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa masuala ya siasa, wasimamizi wa uchaguzi na magavana wa maeneo mbalimbali hapa nchini ameashiria mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ilitaka kufutwa maazimio na vikwazo vyote vilivyopasishwa dhidi yake na si kusimamishwa, na lengo hilo limetimia.

Rais Rouhani amesema mafanikio ya taifa la Iran katika medani ya nyuklia ni miongoni mwa mafanikio makubwa zaidi si kwa taifa la Iran pekee bali kwa nchi zinazostawi mbele ya madola makubwa. Akiendelea kuashiria mafanikio hayo ya Iran, Rais Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kurutubisha madini ya urani, kufanya uhakiki na ustawi wa masuala ya nyuklia na kudumisha shughuli na kazi za kituo cha nyuklia cha maji mazito cha Arak hapa nchini.

Wakati huo huo Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran, Dakta Ali Akbar Salehi amesema kuwa Iran ya Kiislamu sasa imeanza harakati kubwa ya kihistoria ya ustawi na maendeleo.

Akizungumza katika ujumbe wake kuhusu kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia, Dakta Salehi amesema, Jamhuri ya Kiislamu inatarajia kuwa itaanza ujenzi wa kituo cha pili cha kuzalisha nishati ya nyuklia huko Bushehr kusini mwa Iran hivi karibuni.

Jumamosi iliyopita Iran na nchi za kundi la 5+1 zilianza kutekeleza rasmi makubaliano ya nyuklia ambayo yamehitimisha vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)