Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Januari 2016 15:53

Kiongozi ajibu barua ya Rais Rouhani kuhusu JCPOA

Kiongozi ajibu barua ya Rais Rouhani kuhusu JCPOA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu barua aliyoandikiwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu kumalizika mazungumzo ya nyuklia na amesema, amefurahishwa na kuona kuwa pande zilizokuwa zinazungumza na Iran zimelazimika kulegeza kamba na kurudi nyumba mbele ya muqawama wa taifa la Iran na jitihada za timu za mazungumzo za Iran.

Katika majibu yake hayo, Ayatullah Ali Khamenei amemshukuru pia Rais Hassan Rouhani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na watu wote waliohusika kwenye mazungumzo ya nyuklia.

Katika barua hiyo amewatahadharisha maafisa wote wa serikali kwamba, utatuzi wa matatizo ya kiuchumi nchini utapatikana kwa kufanyika jitihada zisizosita na kwa hekima na busara katika sekta zote katika kufanikisha uchumi wa kimuqawama na kwamba kuondolewa vikwazo tu hakutoshi kutatua matatizo ya kiuchumi na kuwaletea maisha bora wananchi.

Katika barua yake hiyo ya majibu kwa barua ya Rais Rouhani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, katika kulitangaza suala hilo, inabidi isisitizwe kuwa taifa limegharamika mno katika jambo hili na kuongeza kuwa, maandishi na matamshi yanayotolewa kwa lengo la kujaribu kufifiliza na kupunguza umuhimu wa uhakika huo na kuonesha kuwa jambo hili limewezekana kutokana na kufadhiliwa na upande wa Magharibi, kwa hakika hayawatendei haki wananchi.

Vile vile amesema katika sehemu moja ya majibu yake hayo kwamba, inabidi ihakikishwe kuwa upande wa pili unatekeleza kikamilifu ahadi zake. Hata hivyo amesema, matamshi ya siku mbili tatu zilizopita yaliyotolewa na baadhi ya wanasiasa wa Marekani yanaifanya Iran kuwa na mtazamo mbaya kikamilifu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)