Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Januari 2016 10:51

Zarif: Saudia inaeneza chuki dhidi ya Iran M/Kati

Zarif: Saudia inaeneza chuki dhidi ya Iran M/Kati

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia unaeneza chuki na propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ili kuibuka taharuki katika eneo la Mashariki sambamba na kufanikisha ajenda zake.

Katika mahojiano na kanali moja ya televisheni hapa nchini, Muhammed Javad Zarif amesema, wasi wasi wote huo wa serikali ya Riyadh umetokana na kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya nyukia ya Iran.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema miongoni mwa mbinu zinazotumiwa na utawala wa kifalme wa Saudia ili kuzusha hofu katika eneo ni hatua yao ya hivi karibuni kushusha bei ya mafuta na kusisitiza kuwa: “Kupunguza bei ya mafuta ina taathira hasi kwao, kulikoni kwetu.

Muhammed Javad Zarif ameongeza kuwa, Saudia haiwezi kufanikisha sera zake kwa kueneza chuki na propaganda dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumamosi iliyopita na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya huko mjini Vienna, Austria, vikwazo vyote vya kifedha, uchumi na vinginevyo vinavyohusiana na mpango wa nyuklia wa Iran vimeondolewa rasmi kuanzia tarehe 16, Januari mwaka huu, kwa mujibu wa makubaliano hayo ya nyuklia yanayojulikana kama JCPOA.

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)