Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Januari 2016 06:42

Mogherini: Kutekelezwa JCPOA ni hatua kubwa

Mogherini: Kutekelezwa JCPOA ni hatua kubwa

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 ni hatua kubwa katika mwelekeo sahihi.

Bi Federica Mogherini amesema ana uhakika kuwa kile walichokifanya Jumamosi wiki hii huko Vienna, Austria ilikuwa ni hatua kubwa kwa ajili ya eneo la Mashariki ya Kati. Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameongeza kuwa kutekelezwa mpango wa JCPOA kumethibitisha kuwa hata yale mahusiano magumu yanaweza kupatiwa natija nzuri kupitia njia za mazungumzo, diplomasia na ushirikiano. Amesisitiza kuwa amani haiwezi kupatikana kwa haraka na kwa urahisi kama ambavyo makubaliano ya nyuklia hayakupatikana mara moja na kwa urahisi. Makubaliano ya JCPOA yalitiwa saini kufuatia mazungumzo ya kina yaliyodumu kwa miaka miwili na nusu kati ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)