Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 20:21

'Ukurasa mpya umefunguliwa baina ya Iran na IAEA'

'Ukurasa mpya umefunguliwa baina ya Iran na IAEA'

Makamu wa Rais na ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (IAEO) amesema kuwa safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hapa Tehran imefungua ukurasa mpya katika ushirikiano kati ya pande mbili.

Akizungumza leo katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari akiwa pamoja na Yukia Amano, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Ali Akbar Salehi Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameongeza kuwa: Hivi sasa hakuna tena suala la faili bandia la nyuklia la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Salehi amesema mtazamo wa pande mbili za Iran na IAEA sasa unapasa kuwa ni wa kuangalia mbele na kusahau yote yaliyopita. Salehi ameongeza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameombwa kuchukua hatua kufidia fursa mbalimbali zilizopotea katika muda wa miaka 12 wa faili bandia la nyuklia dhidi ya Iran zikiwemo fursa za ushirikiano wa kiufundi. Makamu wa Rais wa Iran ameongeza kuwa katika kikao alichofanya na Yukia Amano wamebadilishana mawazo kuhusu namna ya kushirikiana katika siku za usoni hususan katika anga mpya iliyopo na kwamba kiujumla wameweza kuandaa ramani ya njia juu ya suala hilo. Yukia Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa IAEA leo alfajiri amewasili Tehran katika safari yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Iran na wakala huo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)