Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 20:19

Rais amwandikia barua Kiongozi Muadhamu

Rais amwandikia barua Kiongozi Muadhamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza mafanikio iliyopata Iran katika nyuga za kinyuklia, kisiasa, kisheria na kiuchumi.

Barua ya Rais Hassan Rouhani kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imeeleza kuwa: Serikali imedhamiria kufuatilia kwa umakini na kwa azma thabiti na kuona kuwa upande wa pili unatekeleza ahadi zake kwa kuzingatia kikamilifu miongozo ya Kiongozi Muadhamu, na kufelisha njama yoyote ile ya maadui yenye lengo la kutumia vibaya ili kuingilia kati kadhia hiyo. Barua ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Kiongozi Muadhamu imeongeza kuwa: Hatimaye mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta ya nyuklia kutokana na istiqama na kusimama kidete wananchi wa Iran kwa muda wa miaka 12 mbele ya vitisho na vikwazo vyote, na chini ya uongozi wa busara na wa kishujaa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Hivi sasa kumefunguliwa njia ya kustawi uchumi wa Iran kupitia kutekelezwa kikamilifu na kwa azma ya kweli siasa za uchumi wa kimuqawama kufuatia kuondolewa vikwazo hivyo vya kidhulma.

Rouhani amesema: Serikali ina imani thabiti kuwa, hata kama kuondolewa vikwazo hivyo vya kidhulma na kupatikana haki za wananchi wa Iran lilikuwa ni jambo la lazima na la dharura, lakini kustawi uchumi, kuboresha maisha ya wananchi na kupatikana ajira, kutawezakana tu kwa kutekelezwa uchumi wa kimuqawama na kushiriki ipasavyo wananchi wote katika sekta ya uwekezaji, kazi na ubunifu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)