Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 20:18

Ansari: Kutekelezwa JCPOA kutaandaa fursa zaidi

Ansari: Kutekelezwa JCPOA kutaandaa fursa zaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema anataraji kuwa kutekelezwa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kutaandaa fursa nzuri kwa ajili ya ustawi zaidi wa kisiasa na kiuchumi wa taifa la Iran.

Sadeqi Hussein Jaberi Ansari amesema kuwa taifa la Iran linaamini kuwa kutekelezwa kwa makini mpango wa JCPOA ni kiashirio kwa ajili ya masuala yajayo na kwamba, utekelezaji wa ahadi za kimataifa za Marekani na washirika wengine wa JCPOA katika uwanja wa maamuzi ya kusimamia mustakbali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unaweza kuwa na athari nzuri. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo leo hapa Tehran katika kikao cha kila wiki na waandishi wa habari wa ndani na nje.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema pia kuhusu mazungumzo ya simu yaliyofanyika baina ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Marekani; na uwezekano wa kuangaliwa upya uhusiano wa nchi mbili hizi kwamba: Mazungumzo ya simu endelevu yamekuwa yakifanyika katika marhala zote za mazungumzo ya JCPOA hadi kuanza utekelezaji wa mpango huo kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi mbili hizo yaani Marekani na Iran kwa ajili ya kufuatilia kadhia hiyo; na kwamba mawasiliano hayo yanapaswa kutafsiriwa kwa kiwango hicho hicho na kutotolewa tafsri iliyo mbali na hiyo. Kuhusu kuzidishwa vikwazo vya hivi karibuni dhidi ya Iran, Jaberi Ansari amesema kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo inayoratibu mipango yake, kuchunguza na kuchukua uamuzi kuhusu hatua yoyote inayokiuka ahadi na utekekezaji wa majukumu ya kimataifa ya Marekani kwa mujibu wa maamuzi ya tume kuu ya kusimamia utekelezaji wa mpango wa JCPOA ambayo ndiyo marejeo halisi ya uchukuaji maamuzi yanohusiana na JCPOA.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)