Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 11:20

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA aendelea na ziara yake Iran

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA aendelea na ziara yake Iran

Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amewasili leo hapa mjini Tehran kwa nia ya kupanua uhusiano wa wakala huo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa ya wakala huo, Yukiya Amano ataonana na Rais Hassan Rouhani pamoja na Ali Akbar Salehi, Makamu wa Rais na Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran.

Taarifa hiyo ya IAEA imeongeza kuwa, nafasi ya wakala huo itajikita katika kufanyia majaribio na kusimamia utekelezaji wa ahadi za nyuklia za Iran kwa mujibu wa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Jana usiku pia, Ali Akbar Salehi alisema, lengo la safari hiyo ya Yukiya Amano hapa Tehran ni kustawisha uhusiano wa Iran na IAEA. Amesema, miongoni mwa kazi za wakala huo ni kutoa huduma kwa wanachama wake, Iran ikiwa ni wanachama hai wa wakala huo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)