Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 11:20

Algeria: Utekelezaji wa JCPOA mafanikio ya kihistoria

Algeria: Utekelezaji wa JCPOA mafanikio ya kihistoria

Serikali ya Algeria imeipokea kwa furaha habari ya kuanza kutekelezwa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran na kusema kuwa, hayo ni mafanikio ya kihistoria.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imetoa tamko na kusema kuwa, utekelezaji wa makubaliano hayo ya kihistoria ya nyuklia kati ya Iran na madola makubwa duniani ni mafanikio ya kihistoria na inaonesha kupata nguvu ya kujitawala na kujiamulia mambo yake mataifa ya dunia na pia haki ya kila nchi ya kutumia kwa njia za amani teknolojia ya nyuklia.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imeongeza kuwa, utekelezaji wa mpango wa JCPOA ni hatua muhimu ya kukomesha mivutano na migogoro iliyopo na kulindwa amani na usalama kimataifa na pia kufanikisha juhudi za ustawi na maendeleo za mataifa yote.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imeongeza kuwa, kuanza kuondolewa pole pole vikwazo dhidi ya Iran ni mafanikio mengine yaliyomo kwenye makubaliano hayo na inabidi kila upande uoneshe nia yake njema katika jambo hilo.

Hadi hivi sasa nchi nyingi duniani na taasisi za kimataifa zimeelezea kufurahishwa kwao na kuanza utekelezaji wa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kati ya Iran na madola makubwa duniani.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)