Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Januari 2016 05:46

Obama akiri, vikwazo dhidi ya Iran havikufua dafu

Obama akiri, vikwazo dhidi ya Iran havikufua dafu
Rais Barack Obama wa Marekani amekiri kuwa vikwazo vya kidiplomasia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havikuwa na maslahi kwa nchi yake.

Barack Obama amesema kuwa makubaliano ya kihistoria ya nyuklia na Iran ni mafanikio ya kidiplomasia na kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havikuifaidisha chochote nchi hiyo.

Rais wa Marekani lisema jana jioni baada ya kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 kwamba, kumefikiwa mapatano hayo ya nyuklia bila ya vita vipya katika eneo la Mashariki ya Kati. Vilevile ameashiria kuwa Marekani na Iran zimefikia mapatano ya kutatua hitilafu za kifedha zilizokuwepo tangu zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

Hata hivyo Rais wa Marekani amesema nchi hiyo inaendela kutofautiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan kuhusiana na Israel. Vilevile amesema Washington itaendelea kuiwekea vikwazo Iran kuhusu miradi yake ya kuzalisha makombora ya balestiki.

Ikumbukwe kuwa jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alitangaza kuwa nchi hiyo italazimika kuipatia Iran dola bilioni 1.7 kufuatia kesi iliyowasishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Hague nchini Uholazni.

Kerry amesema Marekani na Iran zimefikia mapatano kuhusu faili la ununuzi wa silaha katika muongo wa 1970 ambapo Marekani ilikataa kuikabidhi Iran silaha hizo baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)