Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 17 Januari 2016 11:32

Dunia yakaribisha mapatano ya nyuklia ya Iran

Dunia yakaribisha mapatano ya nyuklia ya Iran

Dunia imepokea vizuri tangazao la Wakala wa Kimataifa wa Nisahti ya Atomiki IAEA kuhusu kufungamana Iran na ahadi zake katika mapatano ya nyuklia sambamba na taarifa ya pamoja ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.

Shirika la Habari la Itar Tass la Russia limetangaza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema mafanikio katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kati ya Iran na madola sita makubwa duniani ni jambo ambalo litadhamini usalama wa Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi. Amebainisha matumaini yake kuwa Iran na nchi sita kubwa duniani zitaweza kutekeleza mapatano hayo ya nyuklia kwa nia safi.

Shirika la AFP nalo limemnukulu Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa akisema mapatano ya nyuklia ya Iran ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia.

Associated Press imemnukulu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA akisema utekelezwaji wa mapatano wa nyuklia ni mwanzo mpya baina ya wakala huo na Iran.

Shirika la Habari la Reuters limenukulu taarifa ya John Kerry Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani akisema 'subira na udiplomasia ni nukta mbili muhimu katika kufanikiwa mazungumzo ya nyuklia ya Iran.'

Shirika la Habri la AFP limeandika kutoka London kuwa, serikali ya Uingereza imepokea vizuri mapatano ya nyuklia na Iran na kusema huo ni mwanzo mpya.

Wakati huo huo Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha utekelezwaji mapatano ya nyuklia ya Iran na kusema hiyo ni hatua muhimu. Aidha ameyataka mapatano hayo ya nyuklia kuwa ni 'mafanikio katika historia ya udiplomasia.'

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu amekariri madai yake yasiyo na msingi na ya kipuuzi dhidi ya Iran. Netanyahu amedai kuwa, pamoja na kuwepo mapatano ya nyuklia Iran inalenga kumiliki silaha za nyuklia. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kuthibitisha kuwa shughuli zake za nyuklia zinafanyika kwa malengo ya amani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)