Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 17 Januari 2016 06:32

Rouhani alipongeza taifa la Iran utekelezaji wa JCPOA

Rouhani alipongeza taifa la Iran utekelezaji wa JCPOA

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelipongeza taifa la Iran kwa mafanikio liliyoyapata katika uga wa nyuklia kwa kuanza kutekelezwa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Alfajiri ya kuamkia leo Jumapili, yaani dakika chache baada ya kutangazwa rasmi kuanza utekelezaji wa mpango huo, Rais Hassan Rouhani ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa hatimaye utekelezaji wa JCPOA umeanza, ninamshukuru Mwenyezi Mungu na ninapenda kusema kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwa taifa kubwa na lenye uvumilivu la Iran na ninatoa mkono wa baraka kwa taifa.

Amesema katika ujumbe wake huo kwamba, jitihada za timu ya Iran ya mazungumzo ya nyuklia katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita kwa ajili ya kufikia kwenye Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) zinapaswa kushukuriwa.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)