Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 17 Januari 2016 06:22

Ujumbe wa nyuklia waondoka Vienna, kurejea Tehran

Ujumbe wa nyuklia waondoka Vienna, kurejea Tehran
Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na timu ya ngazi za juu ya nyuklia ya Iran wameondoka mjini Vienna Austria na kurejea Tehran baada ya kusomwa tamko la pamoja la kuanza utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, baada ya kusomwa tamko la pamoja na taarifa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA mjini Vienna, Austria na kuanza utekelezaji wa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), vikwazo vyote vya kidhulma ilivyokuwa imewekewa Iran kwa kisingizio cha miradi yake ya nyuklia, vimeondolewa.

Yukiya Amano, Mkurugenzi wa IAEA amesema kuwa, ushirikiano wa Iran na wakala huo umeingia katika awamu mpya. Amesema: Leo katika ripoti yangu nimethibitisha kuwa Iran imekamilisha hatua za lazima za awali za utekelezaji wa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na ripoti hii imewasilishwa pia kwa bodi ya magavana wa IAEA na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya wakala wa IAEA kuthibitisha kuwa Iran imetekeleza vizuri ahadi zake, Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya wamesoma tamko la pamoja na kutangaza rasmi kuwa tarehe 16 Januari 2016 ni siku ya kuanza kutekelezwa mpango wa JCPOA.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)