Habari http://kiswahili.irib.ir Sat, 24 Mar 2018 03:17:30 +0430 sw-sw Jumamosi 30 Aprili 2016 http://kiswahili.irib.ir/habari/item/56722-jumamosi-30-aprili-2016 http://kiswahili.irib.ir/habari/item/56722-jumamosi-30-aprili-2016

Leo ni Jumamosi tarehe 22 Rajab 1437 Hijria sawa na tarehe 30 Aprili mwaka 2016 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 239 iliyopita, alizaliwa Carl Friedrich Gauss mwanahisabati na mnajimu mashuhuri wa Kijerumani. Mama yake Gauss ndiye aliyemshawishi mno mwanawe ajikite zaidi katika somo la hisabati, na hatimaye mtoto huyo alitabahari kwenye fani hiyo. Msomi huyo wa hisabati na mnajimu mashuhuri wa Kijerumani alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 78. ***

Katika siku kama ya leo miaka 109 iliyopita, aliaga dunia Sheikh Ja'afar Kashif al-Ghitaa msomi na fakihi mtajika wa Kishia. Alizaliwa mjini Najaf huko Iraq na kuanza kujihusisha na masomo ya dini tangu katika kipindi cha utoto wake. Awali alisoma masomo ya utangulizi kwa baba yake na kisha baadaye akahudhuria masomo kwa wasomi wakubwa wa zama hizo kama sayyid Mahdi Bahr al-Uluum. Baadaye Sheikh Ja'afar Kashif al-Ghitaa alianza kufundisha na kuandika vitabu na kufanikiwa kuwalea wanafunzi wengi na vile vile kuandika vitabu vingi katika nyanja mbalimbali. ***

Tarehe 30 Aprili mwaka 1945 dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler alijiua akiwa mafichoni chini ya ardhi baada na kufeli ndoto yake ya kutawala dunia nzima. Hitler alizaliwa mwaka 1889 nchini Austria na alipigana Vita vya Kwanza vya Dunia katika safu za kwanza za askari wa Ujerumani. Adolf Hitler alianzisha chama cha National Socialist German Workers baada ya kuchanganya itikadi za kisoshalisti na mitazamo mikali ya utaifa. Na ulipotimia mwaka 1939 alianzisha Vita vya Pili vya Dunia.***

Na miaka 191 iliyopita Mullah Ali bin Jamshid mashuhuri kwa jina la Akhund Nuri alimu na msomi mashuhurin aliaga dunia. Mbali na kufundisha alikuwa akijihusisha pia na kazi ya uhakiki. Akhund Nuri alikuwa mahiri pia katika taaluma ya falsafa. Alimu huyo amevirithisha vizazi vilivyokuja baada yake vitabu vingi na vyenye thamani kubwa.***

]]>
Leo katika Historia Sat, 30 Apr 2016 08:48:53 +0430
Algeria yawaachilia wachimba migodi wa Chad http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56720- http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56720- Wizara ya Mambo ya Mahakama nchini Chad imetangaza kuachiliwa huru wachimba mgodi 103 raia wa nchi hiyo ambao walikuwa wakishikiliwa nchini Algeria kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, wachimba migodi hao tayari wameshawasili N'Djamena, mji mkuu wa Chad. Imesema kuwa, watu hao wameachiliwa baada ya Waziri wa Masuala ya Mahakama ya Chad kulifuatilia suala hilo huko Algeria. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Wizara hiyo ya Vyombo vya Mahakama na ambaye hakutaka kutaja jina lake, wachimbamigodi hao wanaojishughulisha na uchimbaji dhahabu katika milima ya Tibesti inayoishia kaskazini mwa nchi hiyo, walitiwa mbaroni na askari wa Algeria mwaka mmoja uliopita na kuzuiliwa nchini humo kwa kipindi chote hicho. Baadhi ya duru zimesema kuwa, wachimba migodi hao wameachiliwa huru kufuatia msamaha wa Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ambaye ameamua kuwasamehe raia hao wa Chad. Wachimbaji hao wadogowadogo wa madini kutoka Chad hupendelea sana kufanya shughuli zao katika milima ya Tibesti, na wakati mwingine wanavuka mmpaka na kuingia Niger na kufika hadi katika ardhi ya Algeria kupitia Nigeri kwa ajili ya kuchimba dhahabu kinyume cha sheria.

]]>
Afrika Sat, 30 Apr 2016 08:42:37 +0430
Kodivaa yawarejesha nyumbani raia wake kutoka Gabon http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56719- http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56719- Wizara ya Mambo ya Nje ya Ivory Coast imetangaza kuwa, imewarejesha nyumbani zaidi ya raia 100 kutoka Gabon kutokana na kuwa na hali mbaya za kimaisha.

Kwa mujibu wa wizara hiyo ya mashauri ya kigeni ya Kodivaa watu 127 kati ya 460 tayari wamerejea nyumbani kwa hiari kutokana na matatizo ya kimaisha. Imeongeza kuwa raia hao ambao awali waliomba kurejea nyumbani kwao, waliwasili jana na ndege maalumu ya serikali mjini Abidjan, mji mkuu wa zamani wa nchi hiyo. Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Ivory Coast imeongeza kuwa, watu hao 127 ni pamoja na watu wazima na watoto. Tarehe tisa Machi mwaka huu, serikali ya Kodivaa ilitangaza azma yake ya kuwarejesha nyumbani raia wake 170 hadi 460 ambao wanaishi katika hali ngumu ya kimaisha nchini Gabon na Angola. Baada ya kurejea nyumbani serikali ya Yamoussoukro ilimpatia kila mmoja wao kiwango fulani cha Frank za nchi hiyo ambazo ni sawa na dola 200 za Kimarekani pamoja na chakula.

]]>
Afrika Sat, 30 Apr 2016 08:41:54 +0430
Libya kuongeza kiwango cha uzalishaji mafuta http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56718- http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56718- Viongozi wa Libya wamekubaliana na mpango wa awamu tatu wa shirika la taifa la mafuta la nchi hiyo wa kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu na kuufikisha katika kiwango cha kabla ya mwaka 2011.

Shirika la taifa la mafuta la Libya lilisema jana (Ijumaa) kuwa lina matumaini - kwa uungaji mkono wa serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo - litaweza kurejesha kiwango cha uzalishaji mafuta nchini humo cha kabla ya kuanza kampeni za kumg'oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi zilizoanza mwaka 2011.

Kiwango cha uzalishaji mafuta nchini Libya hivi sasa ni chini ya robo ya kiwango kilichokuwa kikizalishwa na Libya kabla ya kupinduliwa serikali ya Kanali Muammar Gaddafi. Wakati huo Libya ilikuwa ikizalisha karibu mapipa milioni moja na laki siku kwa siku.

Hata hivyo kurejesha kiwango cha uzalishaji mafuta cha kama ilivyokuwa katika kipindi cha serikali ya Muhammad Gaddafi ni jambo linalohitajia miaka mingi kwani hivi sasa kuna migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi wa taasisi za mafuta, kuna makundi kadhaa yenye silaha yanayodhibiti maeneo tofauti na hakujawa na serikali yenye nguvu ya kudhibiti kila kitu huko Libya.

]]>
Afrika Sat, 30 Apr 2016 08:41:27 +0430
UN yapongeza serikali ya Umoja wa Kitaifa S/Kusini http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56717-un-yapongeza-serikali-ya-umoja-wa-kitaifa-s-kusini http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56717-un-yapongeza-serikali-ya-umoja-wa-kitaifa-s-kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha kuundwa serikali ya عmoja wa نitaifa nchini Sudan Kusini baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kuliapisha baraza jipya la mawaziri na kuzitaka pande husika zikamilishe hatua zote za kuunda taasisi za serikali hiyo ya mpito.

Ban ametoa taarifa hiyo akisema kuwa amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya mahasimu wawili Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar ya kukubali kufanya kazi kwa pamoja na kumaliza mgogoro wa miaka kadhaa wa nchi hiyo. Amesema viongozi hao na pande zote husika zinapaswa kuongeza juhudi za kuukamilisha mchakato mzima wa kuunda taasisi zote za serikali hiyo ya mpito. Aidha amezitaka pande hizo zikomeshe haraka uhasama baina yao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza tume maalumu ya kusimamia zoezi hilo inayojulikana kwa kwa kifupi JMEC ambayo miongoni mwa wajumbe wake ni Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae, na Rais wa zamani wa Mali, Alpha Omar Konare kwa ajili ya kusimamia mchakato wa amani na kuhakikisha kuwa Sudan Kusini inarejea katika usalama, utulivu na maelewano. Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa iendelee kusaidia juhudi za kuleta amani na kuhakikisha kuwa makublaiano ya amani ya Sudan Kusini yanatekelezwa kikamilifu. Itakumbukwa kuwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini ina mawaziri 30 kutoka kwa wafuasi wa Rais Salva Kiir na wa mkuu wa zamani wa waasi, Riek Machar ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais. Riek Machar aliapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini mara baada ya kurejea mjini Juba siku ya Jumanne.

]]>
Afrika Sat, 30 Apr 2016 08:39:35 +0430
Iran: Dunia iungane katika vita dhidi ya ugaidi http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56716- http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56716- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonya kuhusu kuenea ugaidi na misimamo mikali duniani na kusema jamii ya kimataifa inapasa kushirikiana kukabiliana na uovu huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Morteza Sarmadi alipozungumza na waandishi habari baada ya Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kongamano la Maingiliano na Hatua za Kuaminiana ASIA (CICA) mjini Beijing Uchina, Ijumaa.

Ameongeza kuwa kuwa dunia inashuhudia kuongezeka ugaidi, taasubi za kimadhehebu na makudni wa wakufurishaji na hivyo kupelekea hali kuwa ngumu katika nchi nyingi hasa Mashariki ya Kati.

Sarmadiametoa wito kwa nchi za Asia kushirikiana kwani kukabiliana na ugaidi ili eneo hilo lishuhudie amani na usalama. Aidha amebainisah azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano wa nchi za CICA.

]]>
Iran Sat, 30 Apr 2016 08:38:50 +0430
Watu saba wapoteza maisha kufuatia mvua kali Nairobi http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56715- http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/56715- Watu saba wanaripotiwa kupoteza maisha siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kufuatia mvua kali zinazoendelea mjini humo.

Katika tukio la kwanza Ijumaa mchana watu wanne wamefariki baada ya ukuta kuporomoka na kuwaangukia mtaani Kilimani kati ya ubalozi wa Russia na makao makuu ya idara ya ulinzi DOD.

Aidha watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi baada ya jingo la ghorifa sita kuporomoka Ijumaa usiku kufuatia mvua kali. Maafisa wa uokoaji wangali wanaendelea kuwatafuta watu wanaoaminika kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo ambalo inasemkana likuwa na familia 150 ndani yake.

Baadhi ya barabara jijini Nairobi zilifurika na kutatiza usafiri kutokana na mvua inayozidi kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. Barabara iliyoathirika zaidi ni barabara kuu ya Thika maeneo ya Parklands. Mtaa wa South C pia uliathirika huku wakazi wa Komarock pia wakiathirika kwa maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao. Mitaro ya kuelekezxa maji nje ya barabara inasemekana kujaa taka ambayo ilisababisha barabara hizo kufurika, hata hivyo baadhi ya wenyeji wamelalamika kuwa hakuna mipango madhubuti ya kuelekeza maji kwengineko.

]]>
Afrika Sat, 30 Apr 2016 08:37:57 +0430
Radiamali kuhusu jinai ya ubakaji wa balozi wa Saudia huko nchini Romania http://kiswahili.irib.ir/habari/item/56714-radiamali-kuhusu-jinai-ya-ubakaji-wa-balozi-wa-saudia-huko-nchini-romania http://kiswahili.irib.ir/habari/item/56714-radiamali-kuhusu-jinai-ya-ubakaji-wa-balozi-wa-saudia-huko-nchini-romania

Radiamali zimeendelea kutolewa kufuatia balozi wa Saudia nchini Romania kumbaka msaidizi wake na kisha kumuu. Kwa mujibu wa polisi ya Romania, balozi huyo wa Saudia Abdulrahman Bin Ibrahim Al-Rassi alimbaka msichana aliyekuwa msaidizi wake mwenye umri wa miaka 25 kwa jina la Ivan Wilsco raia wa Romania ambaye alikuwa akifanya kazi katika ubalozi huo wa Saudia nchini humo. Kufuatia jinai hiyo serikali ya Bucharest imeingilia kati kadhia hiyo huku ikikitaja kitendo hicho kuwa ni ukandamizaji wa kijinsia uliovuka mpaka. Ni vyema kuashiria kwamba, baada ya balozi huyo kumbaka Ivan, alimuua. Imebaini kwamba, Abdulrahman Bin Ibrahim Al-Rassi, balozi wa Saudia nchini Romania, alimuua msichana huyo kwa kutumia mkanda wa suruali. Uchunguzi wa awali wa madaktari unaonyesha kwamba, kabla ya Ivan kuuawa alibakwa. Mwili wa Ivan ambaye alikuwa mwanafunzi wa elimu ya udaktari, uliokotwa ukielea juu ya maji karibu na kituo cha kuzalisha umeme karibu na ubalozi wa Saudia. Kufuatia hali hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Romania sanjari na kumwita balozi huyo, umempa masaa 48 kuhakikisha awe ameondoka haraka nchini humo. Afisa mmoja wa serikali ya Romania, amenukuliwa akisema kuwa, serikali ya nchi hiyo imeitaka serikali ya Saudia kumuondolea kinga ya udiplomasia balozi wake huyo, ili aweze kupandishwa kwenye vyombo vya mahakama vya nchi hiyo na kujibu tuhuma za ubakaji na mauaji ya msichana huyo Ivan, ingawa Riyadh imepinga ombi hilo. Kwa mara kadhaa sasa wanadiplomasia wa Saudia au wanamfalme wa ukoo wa Aal Saudi, wamekuwa wakihushishwa na jinai mbalimbali ikiwemo kushikwa na mihadarakati na pia tuhuma za kijinsia. Mwaka uliopita msichana mwengine aliyekuwa akihudumu katika ubalozi huo wa Saudia mjini Bucharest, alipigwa na kudhalilishwa kijinsia na maafisa wa ngazi za juu wa Saudia katika ubalozi huo. 

]]>
Mchanganyiko Fri, 29 Apr 2016 21:38:32 +0430
Kura za uchaguzi wa bunge Iran zaanza kuhesabiwa http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56713-kura-za-duru-ya-pili-ya-uchaguzi-wa-bunge-nchini-iran-zaanza-kuhesabiwa-baada-ya-kuongezewa-muda http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56713-kura-za-duru-ya-pili-ya-uchaguzi-wa-bunge-nchini-iran-zaanza-kuhesabiwa-baada-ya-kuongezewa-muda

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran amesema kuwa, zoezi la kuhesabu kura za duru ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Iran limeanza.

Hii ni katika hali ambayo muda wa kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran uliofanyika leo ulikuwa umeongezewa muda hadi saa mbili usiku. Taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani nchini hapa imesema kuwa, upigaji kura umepongezewa muda kutokana na kujitokeza kwa wingi wapigakura, ambapo awali ulikuwa umepangwa umalizike saa 12 za jioni kwa saa ya hapa Iran.

Duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ilianza saa mbili asubuhi katika vituo 55 vya kupigia kura na katika mikoa 21 ya Iran. Katika uchaguzi huu wagombea 136 wanachuana kwa ajili ya kuwania nafasi 68 zilizosalia wazi bungeni. Tume ya Uchaguzi nchini Iran imesema kuwa, jumla ya watu milioni 17 waliotimiza masharti ya kupiga kura, wameshiriki zoezi hilo muhimu hii leo ambapo wamewapigia kura wagombea wanaowataka. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, ushiriki wa wananchi katika duru ya pili ya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Kiislamu yaani bunge hii leo ulikuwa wa hamasa kubwa. Kwa upande mwingine Hussein Dhulfiqaar, Naibu Waziri wa Masuala ya Usalama nchini amesema kuwa uchaguzi wa leo umefanyika katika anga ya amani.

]]>
Iran Fri, 29 Apr 2016 21:36:00 +0430
Muda wa duru ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Iran waongezwa http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56712- http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/56712- Muda wa kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa Baraza la Ushauri yaani bunge, uliofanyika leo umeongezwa hadi saa mbili usiku. Taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani nchini hapa imesema kuwa, upigaji kura umepongezewa muda kutokana na kujitokeza kwa wingi wapigakura, ambapo awali ulikuwa umepangwa umalizike saa 12 za jioni kwa saa ya hapa Iran.

Duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ilianza saa mbili asubuhi katika vituo 55 vya kupigia kura na katika mikoa 21 ya Iran. Katika uchaguzi huu wagombea 136 wanachuana kwa ajili ya kuwania nafasi 68 zilizosalia wazi bungeni. Tume ya Uchaguzi nchini Iran imesema kuwa, jumla ya watu milioni 17 waliotimiza masharti ya kupiga kura, wameshiriki zoezi hilo muhimu hii leo ambapo wamewapigia kura wagombea wanaowataka. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, ushiriki wa wananchi katika duru ya pili ya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Kiislamu yaani bunge hii leo ulikuwa wa hamasa kubwa. Kwa upande mwingine Hussein Dhulfiqaar, Naibu Waziri wa Masuala ya Usalama nchini amesema kuwa uchaguzi wa leo umefanyika katika anga ya amani.

]]>
Iran Fri, 29 Apr 2016 21:26:01 +0430