Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 19:47

Mtoto wa miaka miwili amuua mama yake US

Mtoto wa miaka miwili amuua mama yake US

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili amemuua mama yake kwa kumpiga risasi katika mkasa uliotokea kwenye mji wa Milwaukee katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Polisi, mtoto huyo aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma cha gari alifyatua risasi na kumuua mama yake Patrice Price mwenye umri wa miaka 26 aliyekuwa akiendesha gari hiyo. Ripoti ya Polisi imefafanua kuwa bastola hiyo ambayo inamilikiwa na rafiki wa kiume wa Patrice ilidondoka chini ya kiti cha dereva na mtoto huyo akaikota na kufyatua risasi iliyopenya kwenye kiti cha mbele na kumpata mama yake. Mama wa Patrice pamoja na mtoto mwengine wa kiume wa Patrice mwenye umri wa mwaka mmoja walikuwa wamekaa kiti cha mbele cha abiria, lakini walinusurika katika tukio hilo lilitokea Jumanne asubuhi. Mkasa huo umetokea katika kipindi cha chini ya miezi miwili tangu mama mwengine alipopigwa risasi na kujeruhiwa na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka minne katika tukio linalofanana na hilo katika jimbo la Florida.

Siku hiyo hiyo ya Jumanne asubuhi, mtoto mwengine wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu alijiua kwa bahati mbaya kwa kujipiga risasi katika eneo la Paulding lililoko kwenye jimbo la Georgia nchini Marekani. Kwa mujibu wa Polisi ya eneo hilo Holstone Cole, alijiua kwa kujipiga risasi kifuani baada ya kukuta bastola nyumbani kwao inayoaminika kuwa ni ya baba yake.

Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, kila raia ya wa nchi hiyo anaruhusiwa kubeba silaha.

Maafisa wa Marekani walitangaza mwaka uliopita wa 2015 kuwa bunduki inasababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000 kila mwaka nchini humo. Vifo hivyo vinajumuisha watu wanaouawa kwa bahati mbaya, wanaouliwa kwa kukusudia na wanaojiua wenyewe. Hii ikiwa na maana kwamba katika kila muda wa saa sita, silaha moto huua mtu mmoja nchini Marekani, ambayo ni idadi kubwa zaidi kulinganisha na watu wote waliouliwa katika mwaka mzima wa 2014 katika mashambulio ya kigaidi.../

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …