Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 19:43

HAMAS yatilia mkazo umuhimu wa uungaji mkono wa Iran kwa kambi ya muqawama

HAMAS yatilia mkazo umuhimu wa uungaji mkono wa Iran kwa kambi ya muqawama
Osama Hamdan, Mkuu wa uhusiano wa kimataifa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuna udharura wa kuzidishwa uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kambi ya muqawama ili kupunguza machungu na mateso wanayopata Wapalestina kutokana na muendelezo wa siasa za kidhalimu za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Osama Hamdan ameongeza kuwa uhusiano wa HAMAS na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mzuri na kuongeza kuwa anatumai nchi za Kiarabu pia zitatimiza mas-ulia na wajibu zilionao kwa ajili ya kukomesha mzingiro wa kidhalimu liliowekewa eneo la Ukanda wa Gaza na adui Mzayuni.

Mkuu huyo wa uhusiano wa kimataifa wa harakati ya HAMAS aidha amesema, uhusiano wa maelewano baina ya harakati hiyo na Misri unaendelea vizuri na kubainisha kuwa Hamas inataka kuharakishwa mchakato wa kuboreshwa uhusiano kati yake na Cairo kwa njia ya mazungumzo.

Hapo kabla pia Musa Abu Marzuk, afisa mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Hamas aliashiria kuanza duru mpya ya uhusiano kati ya harakati hiyo na Misri na kusisitiza kuwa mazungumzo baina ya serikali ya Cairo na harakati ya Hamas si ya kuishia kwenye vyombo vya habari tu, bali pande hizo mbili zina mfungamano na maslahi ya pamoja yanayopasa kuzingatiwa.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …