Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 07:06

Waandishi habari waandamana Cairo, 9 wakamatwa

Waandishi habari waandamana Cairo, 9 wakamatwa

Wanachama wa Jumuiya ya Waandishi Habari wamefanya maandamano mjini Cairo wakipinga hatua ya Rais wa Misri, Abdul Fattah al Sisi ya kuipatia Saudi Arabia visiwa viwili vya Tiran na Sanafir na kupasisha makubaliano ya kuchora mipaka ya baharini kati ya nchi hizo mbili.

Medani za Tahrir, Mustafa Mahmoud, al Jalaa na Abididi zimeshuhudia hatua kali za ulinzi sambamba na wito wa jumuiya mbalimbali wa kufanyika maandamano dhidi ya hatua hiyo ya serikali ya Cairo. Waandishi habari 9 wametiwa nguvuni katika maandamano hayo. Askari wa usalama wa Misri pia wamevamia makao makuu ya Jumuiya ya Wandishi Habari na kufunga ofisi zake. Vilevile askari hao wanazingira makao makuu ya Jumuiya ya Madaktari mjini Cairo kwa kuchelea maandamano ya kupinga hatua hiyo ya Rais Abdul Fattah al Sisi.

Maandamano kama hayo pia yameshuhudiwa katika miji mingine ya Misri ambapo wananchi wanapinga kitendo cha serikali ya Cairo cha kuipa Saudia visiwa vya Tiran na Sanafir.

Siku chache zilizopita pia vyama mbalimbali vya Misri kikiwemo chama cha Katiba kinachoongozwa na mkurugenzi wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Muhammad el Baradei vilitoa taarifa vikitangaza kuwa, vimeanzisha kampeni ya wananchi ya kulinda ardhi ambayo imepewa jina la "Misri Haiuzwi".

Taarifa hiyo ilisema kuwa, kampeni hiyo imeanzishwa kupinga hatua ya al Sisi ya kuipatia Saudi Arabia visiwa vya Tiran na Sanafir, na vyama vilivyotia saini taarifa hiyo vimetangaza upinzani wao dhidi ya makubaliano ya kuchora mipaka kati ya Cairo na Riyadh.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …