Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 24 Aprili 2016 19:27

Maadhimisho ya kufeli Marekani jangwani Tabas, Iran

Maadhimisho ya kufeli Marekani jangwani Tabas, Iran
Leo kumefanyika maadhimisho ya kukumbuka kushindwa vibaya jeshi la Marekani katika jangwa la Tabas, mashariki mwa Iran.

Sherehe hizo zimehutubuwa na Brigedia Jenerali Mohammaad Ridha Naqdi, Mkuu wa Taasisi ya Jeshi la Kujitolea la Wananchi la "Basiji Mustadhafina" la Iran ambaye amesema Tarehe 24 Aprili ni kielelezo cha nguvu na irada ya Mwenyezi Mungu SWT. Ameongeza kuwa, tukio la Tabas ni ishara kuwa pamoja na kuwepo kila aina ya mipango, zana na silaha, irada ya Mwenyezi Mungu ya kuunga mkono haki itafikiwa.

Brigedia Jenerali Naqdi ameongeza kuwa, uzoefu wenye thamani wa taifa la Iran unaonyesha kuwa, faili la kuwa na matumaini mema kuhusu Marekani linapaswa kutupwa katika pipa la taka za historia.

Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi la "Basiji Mustadhafina" la Iran ameashiria njama za Marekani na kusema, Jihadi ya leo ni Jihadi ya kiuchumi na taifa la Iran kwa kufuata miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu uchumi wa kimapambano, linaweza kusambaratisha njama za Marekani katika sekta ya uchumi.

Leo Jumapili tarehe 24 Aprili sawa tarehe 5 Ordibehesht miaka 26 iliyopita ni siku ya kukumbuka siku ya kushindwa vibaya hujuma ya Jeshi la Marekani dhidi ya Iran katika Jangwa la Tabas, mashariki mwa Iran. Katika siku kama hii miaka 36 iliyopita, Marekani iliivamia kijeshi ardhi ya Iran kwa kutumia helikopta na ndege kadhaa za kivita. Lakini uvamizi huo ulifeli vibaya kutokana na tufani kubwa ya mchanga iliyotokea Tabas na kupelekea kuanguka baadhi ya ndege, kuwaka moto helikopta za Marekani na kufa baadhi ya askari wa nchi hiyo huku waliobakia wakiikimbia ardhi ya Iran.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …