Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Aprili 2016 12:21

Saudia yakiuka makubaliano ya kusitisha vita Yemen

Saudia yakiuka makubaliano ya kusitisha vita Yemen
Raia wanne wa Yemen wameuawa shahidi akiwemo mtoto mchanga katika mashambulizi yaliyofanywa na vibaraka wa Saudi Arabia dhidi ya makazi na nyumba zao katika eneo la al Zahir kwenye mkoa wa Baidha. Hatua hiyo inatambuliwa kuwa ni ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita unaoendelea nchini Yemen.

Vilevile vibaka wa Saudi Arabia wameshambulia maeneo mbalimbali ya Yemen kama Naham, Asailan, al Waziiyyah na la Amri kwa kutumia silaha nyepesi na nzito.

Wakati huo huo wakazi wa mkoa wa al Jadidah wamepanga kufanya maandamano makubwa kesho Jumapili kulaani mzingiro wa Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen hususan bandari ya al Jadida.

Katika upande mwingine mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen Ismail Ould Sheikh Ahmad amesema baada ya kikao cha kwanza cha mazungumzo ya amani yanayoendelea nchini Kuwait kwamba amewasiliana na Saudi Arabia kuhusu mashambulizi ya anga yanayofanyika nchini Yemen.

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi kufuatia mashambulizi ya Saudi Arabia na washirika wao dhidi ya nchi hiyo ya Kiislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …