Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 22 Aprili 2016 09:08

Wazayuni watumia vibaya mgogoro wa Syria

Wazayuni watumia vibaya mgogoro wa Syria

Licha ya Saudi Arabia kuwa na mielekeo inayofanana na utawala wa Kizayuni katika baadhi ya mambo, lakini mwakilishi wa Saudia katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia vibaya mgogoro wa Syria kujinufaisha binafsi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Ahmad al Qattan alisema jana Alkhamisi katika kikao cha dharura cha jumuiya hiyo kilichojadili misimamo ya hivi kaaribuni ya Israel kuhusu milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni kwamba, inasikitisha kuona kuwa Israel inautumia vibaya mgogoro wa Syria ulioanza miaka kadhaa iliyopita.

Ameongeza kuwa, Saudia na dunia nzima haiwezi kukubaliana na matamshi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni aliyejigamba kuwa milima ya Golan kamwe haitarejeshwa kwa Syria.

Matamshi hayo ya mwakilishi wa Saudi Arabia katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yametolewa katika hali ambayo Riyadh inafuatilia mambo yale yale yanayofuatiliwa na Israel iwe ni katika migogoro ya nchi za Mashariki ya Kati au katika njama za kuyaita makundi ya muqawama kama vile Hizbullah ya Lebanon kuwa eti ni makundi ya kigaidi.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …