Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 18 Aprili 2016 21:24

Wazayuni kadhaa wajeruhiwa mripuko wa bomu Quds

Wazayuni kadhaa wajeruhiwa mripuko wa bomu Quds

Habari kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu zinasema kuwa, Wazayuni karibu 20 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu katika basi moja huko Quds.

Shirika la habari la Reuters limeinukuu polisi ya utawala wa Kizayuni ikitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, basi moja tupu lililokuwa limetegwa bomu limeripuka wakati basi jingine lenye Wazayuni lilipokuwa linapita katika eneo hilo na kupelekea Wazayuni karibu 20 kujeruhiwa. Hadi tunapokea habari hii hakukuwa kumetangaza habari zaidi kuhusu tukio hilo.

Wakati huo huo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeutaka ulimwengu wa Kiislamu kuilinda Quds mbele ya njama za kuuyahudisha mji huo mtakatifu. HAMAS imetoa mwito huo leo kupitia ujumbe wake kwa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa OIC ikimtaka mwenyekiti wa kikao hicho na viongozi wa umma wa Kiislamu waukoe mji wa Baytul Muqaddas mbele ya njama za kuuyahudisha mji huo. Aidha imewataka viongozi wa Kiislamu kuchukua msimamo wa pamoja na ulio wazi wa kuhakikisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaacha mara moja kuuzingira Ukanda wa Ghaza.

Wakati huo huo makuhani waandamizi na taasisi mbalimbali za Kizayuni wametaka kufanyike mashambulizi makubwa dhidi ya Msikiti wa al Aqsa. Shirika la habari la Quds limeripoti leo kuwa, taasisi za Kizayuni zinazoendesha njama za kujengwa maabadi ya Kiyahudi sehemu ulipo Msikiti wa al Aqsa, zimewataka Wazayuni wauvamie kwa wingi msikiti huo, ili waharakishe njama za kubomolewa Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Quds, leo Wazayuni walikuwa na sherehe za sikukuu maarufu ya Mayahudi ijulikanayo kwa jina la Passover huko Deir Yassin, magharibi mwa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu, na makuhani kadhaa waandamizi wamezungumza kwenye sherehe hizo wakiwataka Wazayuni wafanye mashambulizi makubwa kwa lengo la kukibomoa Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …